Mwamko Mdogo Wa Wazazi Kuchangia Vyakula Shuleni , Chanzo Cha Utoro Kwa Wanafunzi Wa Darasa la kwanza
wanafunzi awali wakiripoti shule |
Na Baraka Lusajo – Rukwa
Imeelezwa kuwa ukosefu wa sheria
inayo weza kuwalazimisha wazazi na walezi kuchangia vyakula mashuleni imekuwa chanzo cha wanafunzi wengi wa madarasa ya kwanza na awali mkoani
Rukwa kuwa watoro na wengine kuacha
shule kisha kutumikishwa kwenye shughuli za uvuvi na ufugaji.
Hayo yanajiri siku chache baada shule nyingi za msingi mkoani humo kushindwa kutoa vyakula shuleni ,ambapo hadi kufikia machi 2024 shule 106 za msingi kati 338 mkoani humo zilishindwa kutoa chakula huku chanzo ikidaiwa ni uwepo wa mwamko mdogo wazazi na walezi wa uchangia vyakula shuleni husani kwa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza.
kushoto ni mwenyekiti wa CWT koani Rukwa |
Mwenyekiti wa chama cha walimu (CWT) mkoani
Rukwa Doseph Ndalama, Alisema serikali
haina budi kuanza kufikiria kuupeleka bungeni muswada wa sheria utakao
walazimisha wazazi na walezi kuchangia vyakula shuleni ili kupunguza utoro kwa
wanafunzi na kubainisha kuwa hiyo itasaidia wanafunzi kupenda shule na kusisitiza kuwa zoezi la utoaji chakula shuleni linapaswa kuwa la lazima.
‘’ili tupate watoto watakao kuwa bora
kitaalumu ni lazima wazazi tuwahimize kuchangia vyakula shule na hili lianzie
elimu ya awali ambako ndiko chimbuko la
mtoto la kumjengea uwezo kitaaluma linako anzia.’’ Alisema Ndala.
Kwa upande wake mbunge wa Viti Maalumu
mkoani humo Bupe Mwakang’ata ,Alisema wazazi na walezi wanawajibu wa kulichukua
swala la utoaji vyakula mashuleni kama kipaumbele cha kwanza ili kuinua ufaulu
na taalamu shuleni na kubainisha kuwa wanafunzi wengi wa darasa la kwanza wamekuwa watoro na
kujihusisha na shughuli za ufugaji na uvuvi.
Alisema wao kama wabunge wa mkoa
watahakikisha wanalichukulia swala hilo kwa uzito ikiwezekana kuongea na ofisi
ya mkuu wa mkoa ili kutungwa sheria
ndogo zitakazo wawajibisha wazazi na
walezi wanashindwa kuwapeleka watoto wao shuleni kisha kuwatumikisha kwenye
shughuli za uzalishaji mali ikiwemo ufugaji na uvuvi.
Kwa upande Francis Nkyanduale,
alisema Tanzania ni nchi ya kwanza
katika ukanda wa Afrika mashariki hivyo
kuwepo kwa mazingira rafiki ya kisera kumepelekea ongezeko la ufundishaji
kuongezeka mwaka hadi mwaka na kwamba ili kufikia malengo zaidi serikali haina
budi kuweka utarabu mzuri utakao wezesha wazazi wanaoshindwa kuwapeleka watoto
shuleni kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani.
Kwa mujibu wa afisa taalumu mkoani Rukwa Matinda Mwinuka akiwa ofisini, alisema serikali ya mkoa kwa kushirikiana na walimu wameanza kukaa vikao na kufikia hitimisho la wazazi na walezi kuanza kuchangia vyakula mashul
katika picha ni afisa elimu taaluma mkoa wa Rukwa |
eni na kwamba kwa sasa asilimia 72 ya watoto wa awali na darasa la kwanza wameanza kupata chakula wakiwa shuleni.
‘’ kwa kushirikiana na walimu na viongozi
wa serikali za vijiji na kata tumetoa elimu kwa wazazi na walezi na wameridhia
kuanza kuchangia vyakula shule kwa kutoa debe moja la mahindi , sado moja ya
maharangwe na fedha shilingi elfu kumi kwa kila mwezi .alisema Mwinuka.
Awali akiongea wakati wa tathimini ya
utekelezaji wa mpango wa program jumuishji ya
taifa ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa ngazi ya mkoa, katibu tawala mkoani Rukwa
Gerald Kusaya , aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo kutunga
sheria ndogo zitakazo walazimisha wazazi na walezi kuchangia vyakula mashuleni
na kusisitiza shule zote kuweka mpango
endelevu watoto wa awali kupata chakula.
Licha ya hilo alitishia kuwandikia
barua za kujieleza wakurugenzi ambao watashindwa kutenga bajeti ya fedha
shilingi elfu moja kwa ajili ya uendeshaji wa maswala ya lishe.
Makongoro Nyerere ni Mkuu wa
mkoa wa Rukwa ambapo akiwa ofisni kwake alikiri uwepo wa utoro mashuleni na
kuelezea hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza kwa mwaka 2024 na kubainisha kuwa mkoa ulifanikiwa
kuandikisha watoto wapato elfu thelathini. Ambapo ulilenga kuandikisha
Wanafunzi 57,006 kati yao jinsia ya kiume wakiwa 27,885 na jinsia ya kike
wakiwa 29,121) hadi kufikia tarehe 04 Januari, 2024 Wanafunzi 24,033 wa darasa
la awali sawa na asilimia 42.1 walikuwa wameandikishwa kuanza darasa la awali.
‘’ Kwa upande wa darasa la kwanza Mkoa ulilenga kuandikisha W
anafunzi 51,347 kati yao jinsia ya kiume wakiwa 25,254 na jinsia ya kike wakiwa 26,093) ambapo mpaka tarehe 04 Januari, 2024 Jumla ya Wanafunzi 30,922 walikuwa wameandikishwa kujiunga na darasa la kwanza sawa na asilimia 60.2’’. alisema Makongoro.
Aidha alisesema kwa upande wa
wanafunzi wenye mahitaji maalumu jumla ya wanafunzi wa darasa la awali 167 kati
yao jinsia ya kiume wakiwa 69 na wakike 98) waliandikishwa na kwa upande wa darasa
la kwanza Wanafunzi wenye mahitaji maalumu jumla ya wanafunzi 91, waliandikishwa.
Kaimu
afisa elimu msingi wilayani Kalambo akiwa ofisini kwake Kanuti Mbawala ,alisema
hadi kufikia tarehe 18/1/2024 halmashauri ilikuwa na maoteo ya kuandikisha
wanafunzi wa darasa la kwanza 10,901 kati yao wavulana wakiwa 5,382 na
wasichana 5,519 na kwamba hadi kufikia tarehe 18/1/2-26 halmashauri ilifanikiwa
kuandikisha wanafunzi 9,492 kati yao wavulana wakiwa 4,771 na wasichana 4,721.
‘’Pia
halmashauri tumefanikiwa kuandikisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu 4 kati
yao wavulana wakiwa ni 1 na wasichana wakiwa 3, ambapo hadi kufikia sasa
halmashauri imefanikiwa kufikia asilimia 87 ya uandikishaji.’’alisema Kanuti.
Alisema Kwa upande wa wanafunzi wenye mahitaji
maalumu jumla ya wanafunzi wa darasa la awali 167 kati yao jiansia ya kiume
wakiwa 69 na wakike 98) waliandikishwa na kwa upande wa darasa la kwanza kwa
wanafunzi wenye mahitaji maalum jumla ya wanafunzi 91, waliandikishwa na kuanza
masomo.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Lazaro
Komba akiwa ofisni kwake, alisema wilaya
ya Kalambo imefanikiwa kukamilisha vyumba 39 vya madarasa vyenye thamani
ya shilingi billion 1.3 kwa ajili ya
wanafunzi wa awali na kubainisha kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha
wanafunzi wote wanaripoti shule na kuendelea na masomo.
Mkuu wa wilaya Nkasi Peter Lijualikali akiwa ofisini kwake, alisema
wanafunzi wote waliokuwa wameandikishwa wameripoti shule na kundelea na masomo
na kuipongeza serikali kwa kukamilisha vyumba vya madarasa ambavyo vimewezesha
wanafunzi wengi zaidi kuanza masomo kwa mwaka 2024.
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa
Rukwa akiwemo Brown Mtawa ambao licha ya kuipongeza serikli kwa kuwekeza fedha
nyingi kwenye ujenzi vyumba vya madarasa ,waliishauri serikali kuona uwezekano
wa kuongeza idadi ya walimu wa shule za msingi ili kuendana na ongezeko
la madarasa na wanafunzi wanao ripoti shule.
Awali akiongea ofisini kwake
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kalambo shafi Mpenda ,alisema pamoja na mambo mengine halmashauri kushirikiana
na TAMISEMI imeanzisha
mpango wezeshi wa kuwatambua wanafunzi
wa shule za msingi wasio jua kusoma ,kuandika na kuhesabu kutokana na wanafunzi 2,470
wa darasa la kwanza na la pili kushindwa kumudu KKK.
Alisema kwa mwaka 2023 wanafunzi 1,546 wa
darasa la kwanza sawa na asilimia 12 walionekana na kushindwa kumudu kusoma ,
kuandika na kuhesabu huku wanafunzi 10,527
waliweza kumudu KKK yaani kusoma kuandika na kuhesabu kupitia
program maalumu ya kuhakikisha wanafunzi wote wa darasa la kwanza wanamudu KKK.
Amesema
licha ya hilo wanafunzi 10,667 kati yao wanafunzi
11,591 wa darasa la pili walibainika
kumudu kkk huku wanafunzi 924 sawa na
asilimia 8 wakishindwa kumudu KKK na kuongeza
kuwa jumla ya wanafunzi 8,976 wa darasa la tatu sawa na asilimia 90
walibainika kumudu Lugha ya kingereza huku wanafunzi 976 sawa na asilimia 10
walishindwa kumudu lugha ya kingereza.
Hata hivyo
baadhi ya wadau wa elimu kutoka taasisi zisizo kuwa za kiserikali akiwemo Mosses Mwangata, waliishauri serikali kuona uwezekano wa kupeleka muswada bungeni ili kutungwa sheria itakayo walazimisha wazazi
na walezi kuwapeleka shule ikiwemo kukamtwa kwa wanao kaidi.
Hata hivyo
Tanzania ni nchi ya kwanza kwa ukanda wa afrika mashariki katika kuifanya elimu ya awali kuwa ya lazima
ambapo katika sera ya elimu ya mwaka 2014 ili jumuisha elimu ya awali katika
elimu ya msingi kwa kuzitaka shule zote za msingi kuwa na darasa la elimu ya
awali kwa watoto wa chini ya miaka 5.
Aidha uwepo
wa mazingira rafiki ya kisera kumepelekea ongezeko la uandikishaji wa watoto
katika elimu ya awali kufikia 500,000 ndani ya mwaka mmoja kutoka 1,069,823
mwaka 20215 mpaka 1,562,770 mwaka 2016. Aidha kumekuwa na upungufu wa walimu wa
awali ambapo wengi wao wamekuwa
wanaujuzi wa elimu ya msingi na sio elimu ya awali
Licha ya hilo mwaka 2018 wizara ya elimu sayansi
na technolojia iliripoti upungufu wa asilimia 31.7 ya walimu wa elimu ya awali wenye
vigezo katika shule za serikali kutoka walimu 7,861 mwaka 2017 mpaka walimu
5,367 mwaka 2028.
Comments
Post a Comment