DC KALAMBO ; MGAMBO WAJIEPUSHE NA VITENDO VIOVU.

 


Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt.Lazaro Komba amewataka vijana wanaohitimu mafunzo ya jeshi la akiba wilayani humo kuyatumia mafunzo waliyoyapata katika kulinda raia na mali zao ikiwemo kujiepusha na vitendo viovu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao.

Ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya jeshi la akiba yaliyofanyika katika kata ya Mkowe wilayani humo na kushirikisha vijana 143 kati yao wakiume wakiwa 99 na wakike 44 huku kati ya hao vijana 117 wakishindwa kumaliza mafunzo hayo kutokana na sababu mbalimbali.

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wamesema wamefanikiwa kujifunza mbinu mbalimbali za kivita ikiwemo ulengaji shabaha, pamoja na kushiriki shughuli mbambali za kijamii kama vile kujenga majengo ya serikali.

Comments