ASKARI MGAMBO KALAMBO WAPATIWA MAFUNZO YA UCHAGUZI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


 Jeshi la polisi mkoani Rukwa limetoa wito kwa askari wa Jeshi la akiba walioteuliwa kushiriki usimamizi wa uchaguzi Serikali za mitaa utakaofanyika mwezi Novemba, 27/2024 kuzingatia Sheria na miongozo iliyotolewa na Serikali wakati wa uchaguzi huo ikiwemo kujiepusha na vitendo vya Rushwa.

Hayo yamebainishwa na Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Mkoani Rukwa ACP Zacharia Bula wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo askari 252 wa jeshi la akiba Wilayani Kalambo na kusisistiza wasimamizi wa uchaguzi kufanya kazi hiyo kwa weledi ili kufikia malengo ya Serikali katika kufanikisha zoezi hilo.

Kwa upande wake mratibu mwandamizi wa jeshi la polisi mkoani humo Bw. Abd Mchome ametumia fursa hiyo kuwataka wasimamzi wa uchaguzi kuweka kipaumbele kwa wazee na watu wenye ulemavu wakati wa zoezi hilo.


Kwa upande wake kaimu msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Kalambo Ndugu.  Amandus Mtani aliwataka askari hao kuzingatia maelekezo yaliotolewa na Serikali ikiwemo kutofanya kazi hiyo kwa mazoea na kwamba uchaguzi huo utafanyika katika Kata 23 zenye vijiji 111.

Comments