Na Baraka Lusajo – Rukwa
Imeelezwa kuwa imani potofu kwa waumini wa makanisa ya Whatch tower juu ya masuala ya chanjo imekuwa chanzo cha waumini hao kugomea watoto wao kupata chanjo mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali ili kuwalinda watoto wenye umri kuanzia miezi 9 hadi 59.
Katika picha ni waumini wa kanisa la whatch tower katika kijiji cha Kalambo wakigomea zoezi la chanjo ya Surua na Rubella mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. |
Andrea Mwakalinga ambaye ni
askofu msaidizi wa makanisa ya (FPCT) mkoani Rukwa akiwa ofisini kwake, alisema
elimu ya chanjo kwa watoto bado
inahitajika kwani kanisa la Whatch tower limekuwa likipinga chanjo hiyo kwa
muda mrefu licha ya kujua kuwa kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria za
Tanzania na kusisitiza idara za afya
kuwekeza zaidi katika utoaji wa elimu.
Hata hivyo waumini wa kanisa
hilo katika kijiji cha Kalambo kilichopo
mpakani kati ya nchi ya Tanzania na Zambia wilayani Kalambo waligomea watoto
wao wenye umri kuanzia miezi 9 hadi 59 kupata chanjo ya Surua na Rubella ambayo
zoezi lake lilianza kufanyika tarehe
15/2/2024 na kusababisha watoto 9 kutoka kwenye familia za watu wanaoabudu kwenye kanisa hilo kutokupata
chanjo hiyo.
Kiongozi wa kanisa hilo Pascal Joseph, alisema wamegomea watoto wao kupata chanjo hiyo kutokana na zoezi hilo kuwa kinyume na maadili ya kanisa lao na kubainisha kuwa tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo wamekuwa wakigomea mazoezi yote ya chanjo ikiwemo chanjo ya polio na chanjo zingine.
Katika picha ni mkuu wa wilaya ya Kalambo Lazaro Komba akiwa ofisini kwake |
Aliongeza kwa kusema kuwa
watoto wote ambao walishindwa kupatiwa chanjo kutokana na upinzani kutoka kwa wazazi wao, wamewekewa utaratibu maalumu
utakaowawezesha kupata chanjo na kusema zoezi hilo ni la kitaifa na lengo la
serikali ni kuhakikisha watoto wote wenye umri kuanzia miezi 9 hadi miezi 59
wanapata chanjo.
Alisema kila mwaka changamoto
ya waumini wa makanisa hayo kugomea mazoezi ya chanjo yamekuwa
yakijitokeza ambapo kwa mwaka huu
changamoto hiyo ilijitokeza zaidi katika vijiji vya Kaluko, Kalambo na Kasanga na kwamba tatizo lilianzia kwenye
chanjo ya polio ambayo ilikuwa ikihusisha watoto wenye umri wenye umri wa miezi
9 hadi 59.
Kwa upande wake mganga mkuu wa
wilaya hiyo DKT Emanuel Mhanda akiwa ofisini kwake, alisema kuanzia mwezi
Januari 2023 hadi kufikia mwezi februari 2023 watoto 250 waligundulika kuwa na
ugonjwa wa Surua na Rubella na kwamba ugonjwa huo ulianzia katiika vijiji vya Tunyi, Ilonga na badae kuenea zaidi katika vijiji cha Msanzi ambako watoto
16 waligundulika kuwa na ugonjwa huo.
Alisema kwa kutambua umuhimu wa
zoezi hilo kwa kushirikiana na wizara ya Afya walianzisha kampeni ya kutoa
chanjo nyumba kwa nyumba kwa watoto kuanzia miezi 9 hadi 59 na kufanikiwa kutoa
chanjo kwa watoto 45,274 sawa na asilimia 105 dhidi ya walengwa 42,805 katika
vijiji 111 vya wilaya hiyo huku lengo ikiwa ni kuwakinga watoto kupata maambukizi
ya ugonjwa huo kutokana na kuenea sehemu
mbalimbali.
Alisema kwa kutambua hilo wameanzisha mpango wa kutoa elimu nyumba kwa nyumba kwa wazazi na walezi sambasamba na kuyakutanisha makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini ambao watawezesha kusambaza elimu hiyo kwa waumini wao makanisani juu ya umuhimu wa zoezi hilo.
Awali akiongea ofisini kwake kamanda wa jeshi l
Katika picha ni kamanda wa polisi mkoani Rukwa Shrack Masija akiwa ofisini kwake. |
Katika picha ni mkurugenzi wa shirika la Vipamaru mkoani Rukwa akizungumza na vyombo vya habari . |
Alisema serikali ya Tanzania kupitia sera ya afya ya mwaka 2017 imewekeza katika kuboresha uhai wa mama na mtoto kupitia utoaji wa huduma za afya bure kwa akina mama wajawazito ,na watoto chini ya miaka 5. Aidha mpango huo umeweka mazingira wezeshi ya kupunguza magonjwa na vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano kwa kutoa huduma bora.
Hata hivyo uwekezaji wa
serikali ya Tanzania katika uhai wa mtoto unaonekana dhahiri kwenye
kupungua kwa vifo vya watoto kati ya mwaka 2010 na 2015 ambapo kiwango cha vifo
vya watoto wachanga kuazia miezi 0-28 vimepungua kutoka vifo 40 hadi 25 kwa kila
vizazi hai1000 huku vifo vya watoto wachanga kuanzia miezi 0-28 vikipungua kutoka
vifo 99 hadi 43 kwa kila vizazi hai.
Comments
Post a Comment