Mbunge wa Kenya atimuliwa bungeni na mtoto wake mchanga

Bi Zuleika Hassan aliingia bungeni na mwanae mwenye umri wa miezi mitano aliambiwa na mwakilishi wa Spika si mahala sahihi pa kumlelea mtoto wakeHaki miliki ya pichaBUNGE LA KENYA
Image captionBi Zuleika Hassan aliingia bungeni na mwanae mwenye umri wa miezi mitano aliambiwa na mwakilishi wa Spika si mahala sahihi pa kumlelea mtoto wake
Shughuli za bunge la taifa Kenya zilisitishwa Jumatano baada ya mbunge wa kiti cha wanawake kaunti ya Kwale kuingia bungeni na mtoto wake.
Bwana Christopher Omulele, ambaye alikuwa anahudumu kama Spika alimuamuru Bi Zuleikha Hassan ambaye alikuwa ameingia na mwanae mwenye umri wa miezi mitano kuondoka bungeni, akisema kuwa bunge sio mahala sahihi pa kumlelea mtoto wake.
''Nimefukuzwa bungeni kwasababu nilimpeleka mtoto bungeni...niliamua niende kazini na mtoto wangu, mtoto asingebaki peke yake, au nikae nae nyumbani nisiende kazini'', amesema Bi Hassan katika mazungumzo na BBC baada ya kufukuzwa na mwanawe.
Baadhi ya wabunge wanaume na wanawake, hata hivyo waliunga mkono hatua ya Bi Zuleikha kumleta mtoto wake bungeni na wakamtaka aendelee kubakia ndani ya bunge na hivyo kusababisha kusitishwa kwa shughuli za bunge.
Spika aliamua kumuita afisa wa usalama wa bunge kumuondosha Bi Hassan ambaye wakati huo alikuwa amezingirwa na wabunge wenzake wanawake.
Bi Zuleika Hassan na mtoto wake baada ya kufurushwa bungeni
Image captionBi Zuleikha Hassan na mtoto wake baada ya kufurushwa bungeni
"Ingawa ana haki ya kumtunza mtoto wake, hapa sio mahali panapofaa, Kwa hiyo ninaagiza uondoke mara moja ndani ya bunge," aliamuru Bwana Omulele.
''Nilipata dharura leo asubuhi na ikanibidi nije na mwanangu bungeni''.
" Nilikuwa na dharura na nikaamua nisikose kazi nije pamoja na mwanangu. Mwanangu sio bomu la atomiki ambalo linaweza kulipuka," Amesema Bi Hassan.
Kwa nini nikose kazi eti kwasababu ya kuwa na mtoto, nitaomba ruhusa mara ngapi?. Kwani mtoto ni ugonjwa au ni maambukizi?, kwanini tuwatenge akina mama kwasababu ya kuwa na mtoto? Kuzaa ni jambo la kawaida. Kwani kuwa na mwanamke ni shida? alihoji Bi Hassan katika mazungumzo na BBC.
Mwaka 2013 wabunge walipitisha muswada ulioagiza tume ya huduma za bunge kutenga chumba mahsususi (PSC) katika majengo ya bunge kwa ajili ya wabunge wanawake kuwanyonyeshea watoto wao.

Mbunge wa Kenya atimuliwa na mwanae bungeni


Mbunge wa Kenya atimuliwa na mwanae bungeni
Mbunge wa Ijara, Sophia Abdi Noor amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kwamba tukio hilo limetokea katika bunge ambako sheria zinatungwa na akasema anajiuliza hatma ya akina mama wanaofanya kazi nchini Kenya.
"Mtoto huyu ana haki, kama hawatengi chumba basi tutawaomba wanawake wenye watoto wanaonyonya kuja na watoto wao bungeni ili kutuma ujumbe ," Amesema Bi Noor.
Baadhi ya wabunge wanawake walihoji ni kwanini tume ya huduma za bunge limeshindwa kuwapatia kipaumbele wanawake wanaonyonyesha kwa kuwatengea chumba chao maalum cha kunyonyesha.
"Wabunge lazima waongoze kwa mfano na leo tunasema hii inatosha ," amesema mmbunge mmoja mwanamke.
Kupitia mitandao ya kijamii watu mbali mbali wameelezea hisia zao kuhusiana na kisa cha Bi Hassan kwenda bungeni na mwanae.
Colnelius katika ujumbe huu wa twitter anasema katika mabunge mengine duniani, kunyonyesha mtoto sio tatizo, hata mama anapotoa hoja anaweza kuendelea kunyonyesha mwanae.
James Amosa pia kwenye ukurasa wake wa Twitter analinganisha Kenya na Australia kuhusu nafasi ya wabunge wanawake na suala la kunyonyesha watoto wanapokuwa bungeni
Akisema ni aibu kwa bunge la taifa kumfukuza Zuleikha Hassan , na kuongeza kuwa 'mama zetu na watoto wetu wachanga lazima waheshimiwe'.
Nchini Kenya kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi, Safaricom, ndio inayopigiwa upatu kama mfano bora wa kampuni inayojali maslahi ya akina mama kwa kuwatengea sehemu maalum kwa ajili ya kuwawezesha akina mama wanaofanyia kazi katika kampuni hiyo kuwanyonyesha watoto wao wanapokuwa kazini.
Kampuni hiyo ikivitaja vyumba hivyo kuwa ni muhimu.
Yaya wa Uganda akimlea mtoto
Image captionYaya wa Uganda akimlea mtoto
Je hali ikoje kwa wanawake wengine duniani?
Mnamo mwezi wa Novemba, 2015, Bunge la Uganda lilizinduaa kituo kipya ambapo wabunge pamoja na watumishi wa bunge wamekuwa wanakitumia kuwanyonyesha watoto wao, kikiwa ni kituo cha kwanza nchini Uganda kuweka kituo kama hicho katika nafasi za kazi.
Spika wa bunge la Uganda Rebecca Kadaga, alisema taasisi hiyo inaweka mfano wa kuigwa na taasisi zote za serikali na hata za kibinafsi nchini humo.
Hata hivyo ni makampuni machache nchini Uganda yenye mahala palipotengwa kwa ajili ya unyonyeshaji wa watoto wa mahala pa kazi.
Uelewa wa wengi kuhusika na utoaji wa huduma hiyo au kumshughulikia mtoto mchanga kama vile wa miezi miwili ni finyu mno.
Likizo ndefu kwa mama mjawazito inayotolewa na kampuni nyingi ni karibu siku 90.
Hii ni safari ya kwanza ya kimataifa kwa mtoto Neve tangu alipozaliwa Juni 21Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionHii ni safari ya kwanza ya kimataifa kwa mtoto Neve, tangu alipozaliwa Juni 21
Mwaka jana, Waziri mkuuu wa New Zealand, Jacinda Ardern aliingia ndani ya kongamano la Umoja wa mataifa mjini New York akiwa na mtoto wake mchanga.
Japo aliandamana na mpenzi wake Clarke Gayford, Bi Ardern alichukua muda kumchezesha mwanawe mchanga kwa jina Neve Te Aroha, kabla ya kuhutubia baraza kuu la Umoja wa mataifa.
Msemaji wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric, amesema "Waziri mkuu Ardern ni kielelezo chema kwa taifa lake na hatua yake ya kuhudhuria mkutano huo akiwa na mwanawe ni ishara wazi kwamba hakuna mwakilishi bora zaidi kwa nchi kuliko mama mchapa kazi''.
Bwana Dujarric, aliongeza kuwa viongozi wanawake duniani ni 5% kwa hiyo wanahitaji kujisikia huru kadiri ya uwezo wao.
Seneta Larissa Waters akimnyonyesha mwanae bungeniHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSeneta Larissa Waters akimnyonyesha mwanae bungeni
Nchini Australia Wanawake wabunge wanaruhusiwa kunyonyesha wakati vikao vya bunge vikiendelea.
Mnamo mwaka 2016 bunge la nchi hiyo ilijiunga na seneti kuruhusu kunyonyesha, lakini hakuna mbunge ambaye alifanya hivyo hadi mwaka 2017 ambapo Seneta Larissa Waters alikuwa mwanasiasa wa kwanza kunyonyesha katika bunge la taifa hilo.
Bi Waters kutoka chama cha mrengo wa kushoto cha Green Party alimnyonyesha mwanawe wa miezi miwili Alia Joy wakati wa shughuli ya kupiga kura ikiendelea bungeni.
Bunge la uskochi pia linaruhusu wanawake wabunge wenye watoto wanaonyonya kuwanyonyesha wakati vikao vya bunge vikiendelea.
Mbunge wa Japan Yuka Ogata alipoingia bungeni na mwanae , mtoto wake alichukuliwa kama mgeni, ili hali wageni hawaruhusiwi kuhudhuria vikao vya bungeHaki miliki ya pichaNHK
Image captionMbunge wa Japan Yuka Ogata alipoingia bungeni na mwanae , mtoto wake alichukuliwa kama mgeni, ili hali wageni hawaruhusiwi kuhudhuria vikao vya bunge
Nchini Japan wabunge wanawake hawaruhusiwi kuwaleta watoto wao bungeni.
Mwanasiasa nchini Japan alikosolewa na wabunge mwaka 2017 kwa kujaribu kumleta mtoto wake mchanga katika kikao cha bunge.
Yuka Ogata alisema kuwa alitaka kuonyesha kiwango cha masaibu wanayoyayapitia wanawake wanaofanya kazi na kuwatunza watoto wao wakati 

Comments