NAIBU WAZIRI UTUMISHI WA UMMA ATEMBELEA MRADI WA MITI YA TASAF

 


Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejiment ya utumishi wa umma na utawala bora Deus Sangu ametembelea mradi wa miti katika kijiji cha Singiwe kata ya lyowa wilayani Kalambo mkoani Rukwa ulioanzishwa na wanufaika wa mradi wa TASAF wenye ukubwa wa hekali mbili utakao wawezesha kujikwamua na hali ya kiuchumi.


Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo mwenyekiti wa usimamizi wa mradi huo Dismas Nkanga, amesema mradi huo umegharimu fedha shilingi 675,000/= na kwamba miche 2,250 imepandwa.

Mapema akiongea na wakazi wa vijiji hivyo Mhe.Deus Sangu ametumia fursa hiyo kuzitaka halmashauri zote nchini kutoa vipaumbele vya utoaji mikopo ya asilimia 10 kwa wanufaika wa TASAF kupitia vikundi vyao.

Comments