Rais wa jamhuri
ya mungano wa Tanzania Mhe .Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya
kikazi ya siku mbili mkoani Rukwa kuanzia tarehe 15 hadi 17 Julai 2024 kwa
kuzindua miradi 10 ya maendeleo ikiwa ni mara yake ya kwanza ya kutembelea mkoa wa Rukwa tangu
aapishwe kuwa Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania .
Mkuu wa mkoa wa
Rukwa Makongoro Nyerere akiwa ofisini
kwake amesema Mh. Rais atazindua hosptali ya Wilaya ya Nkasi, barabara ya
Sumbawanga – Kasanga, chuo cha ualimu Sumbwanga, chuo cha Veta cha Sumbawanga, ujenzi wa ghala/vihenge vya kuhifadhia nafaka
(NFRA) Sumbawanga na uzinduzi wa jengo la utawala la ofisi ya Mkurugenzi
Mtendaji Halmshauri ya Kalambo.
Aidha amesema
licha ya hayo Mh.Rais pia ataweka mawe ya msingi katika miradi mitano ikiwemo
mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege Sumbawanga, Jengo la chuo cha MUST, Barabara
ya kiwango cha lami ya Kaengesa, na ujenzi wa shule ya wasichana ya Laela
(Rukwa Girls) na baadae kufanya mkutano mkuu wa hadhara na wananchi katika uwanja
wa Nelson Mandela katika manispaa ya sumbawanga.
Hata hivyo
Mh.Rais kwa mara ya mwisho alitembelea mkoa wa Rukwa mwaka 2020 wakati wa
kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais ,wabunge na madiwani, wakati huo Mh.Rais
Dkt.Samia Suluhu Hassan alikuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya mungano wa
Tanzania na mgombea Mwenza.
Comments
Post a Comment