HALMASHAURI ZA MKOA WA RUKWA ZATAKIWA KUANZSHA VITUO VYA UWESHAJI WANANC...

Halmashauri za mkoa wa Rukwa zimetakiwa kuanzisha vituo vya uwezeshaji Wananchi kiuchumi ambavyo vitawawezesha Wakulima kuongeza wigo wa thamani ya mazao yao na kupata masoko kwa urahisi katika nchi za jirani ikiwemo Kongo, Zambia na Burundi.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Baraza la uwezeshaji Wananchi kiuchimi Taifa Prof. Aurelia Kamuzora, wakati wa ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa vituo vya uwezeshaji Wananchi kiuchumi  mkoani Rukwa na kusisitiza Wakurugenzi mkoani humo kutenga fedha kwa ajili ya uanzishaji wa vituo  hivyo  vitakavyo wawezesha Wananchi kujikwamua kiuchumi kwa kupata elimu, mikopo na kuongeza thamani ya mazao yao.

Katibu  mtendaji wa baraza hilo nchini  Beng’i Issa amesema lengo  la Serikali ni kuhakisha Wakulima wananufaika na kilimo chao kwa kuyaongezea thamani mazao yao kisha kuyauza  katika masoko makubwa yaliyopo katika Nchi za jirani  kwa kuweka Nembo  ya Tanzania.

Kwa upande wake Brigedia Jenerali mstaafu Aloyce Mwanjile alitumia fursa hiyo kuwataka Wataalamu kuongeza juhudi katika suala la utoaji elimu kwa Wananchi juu ya namna bora ya uongezaji thamani mazao yao.

Comments