Wakurugenzi mkoani Rukwa watakiwa kuongeza kasi ya makusanyo mapato ya ndani

 

Mwenyekiti wa ALAT mkoani Rukwa Kalolo Ntila amewataka wakurugenzi kuzitumia vizuri fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ili ziweze kuleta tija katika jamii na kusisitiza kuwekwa utaratibu maalum utakao wezesha kuanzishwa miradi itakayo jengwa kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.

Ameyasema hayo kupitia kikao cha ALAT kilichofanyika kwa ngazi ya mkoa katika halmashauri ya kalambo mkoani Rukwa na kuwataka wakurugenzi mkoani humo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ikiwemo kuanzisha vyanzo vipya vya mapato ili kufikia malengo ya serikali katika ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.

 Mapema wakiongea kupitia kikao hicho mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kalambo Shafi Mpenda amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024 hadi kufikia tarehe 15/4/2024 halmashauri ilipokea fedha  kiasi cha shilingi 5,780,828,450,63 kutoka serikali kuu kupitia fedha za ndani na nje kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo  ikiwemo miradi ya afya na utawala .

Aidha amesema hadi kufikia mwezi machi 2024 pekee halmashauri imetumia kiasi cha Tshs 133,159,359,305 .00 kwenye miradi ya maendeleo na kufanya jumla ya matumizi kuanzia julai 2023 hadi machi 2024  kuwa Tshs 4,959,853,548,74 sawa na asilimia 46

kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya  manispaa ya Sumbawanga   KulaNGA Kanyanga ,amesema  halmashauri ya manispaa hiyo imefanikiwa kusambaza madawa na vifaa tiba katika zahanati 28 vituo vya afya na hospitali ya wilaya ikiwa ni pamoja na kukamilisha miundombinu mipya ya kutolea huduma katika shule za msingi na sekondari.

Comments