Na. Zillipa Joseph, Katavi
Katibu Tawala wa wilaya ya
Tanganyika mkoani Katavi Geofrey Mwashitete ameitaka jamii kujenga mazoea ya kuwahusisha
watoto katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo utunzaji wa mazingira hali
itakayopelekea manufaa makubwa kwa nchi kwa nyakati za sasa na zijazo
Mwashitete ametoa kauli hiyo katika kilele
cha wiki ya mazingira wilaya iliyofanyika katika shule ya msingi Kapemba kata
ya Mishamo wilayani humo
Alisema sehemu mojawapo ya kufikisha
ujumbe kwa jamii nzima ni kuhusisha watoto hasa wenye umri mdogo kwani wao wanashika
sana wanachoambiwa
“Hawa watoto ukiwaambia wanabeba hivyo
hivyo lilivyo, sio watu wazima wana mambo kibao kichwani, kwa hiyo hawa watoto wakihusishwa
ipasavyo hakika kutakuwa na mabadiliko chanya siku zijazo’ alisema Mwashitete
Mwashitete amekabidhi miche 3,000 ya
miti ya matunda kwa watoto hao ili ikapandwe katika mazingira wanayoishi
safi sana
ReplyDelete