Wanawake 119 Wajifungua Kwa Njia Ya Upasuaji Hosptali Ya Wilaya Ya Kalambo

 Hospitali ya wilaya ya kalambo mkoani Rukwa kwa kipindi cha miezi sita imewezesha wanawake 860 kujifungua kati yao wanawake 741wakijifungua kwa njia ya kawaida na 119 wakijifungua kwa njia ya upasuaji huku vifo vya mama na mtoto vikipungua kutoka 11-8 kwa mwaka 2023.

Hayo yamebainishwa na mratibu wa huduma za mama na mtoto wilayani humo Bakari Ndarusi wakati wa utoaji elimu ya kwa wanawake wanao jifungua katika hosptali hiyo,ambapo amesema licha ya hilo hospitali hiyo inahudumia wastani  wa watoto 180 hadi 200 na watoto njiti 6 kwa kila mwezi.

Aidha amesema hosptali hiyo inahudumia wanawake wanaojifungua  wapatao 8-9 kwa siku na kubainisha kuwa hadi kufikia mach 2024 wanawake  2218 wamepatiwa huduma  za mama na mtoto na kwamba kila mwezi wanawake 164 wamekuwa wakihudhuria huduma hizo .

Kwa upande muuguzi mkuu wa hosptali hiyo , Diana Didi amesema licha ya hilo hospitali hiyo imekuwa ikihudumia wanawake 30 kwa siku na kuwataka wanawake kujenga mazoea ya kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya  pindi wanapopatwa na uchungu wa kujifungua ili kuokoa
vifo vya mama na mtoto. 

Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sunday Wambula akiwa ofisni kwake amebainisha kuwa licha ya hilo halmshauri imepokea fedha million mia nne kwa ajili ya umaliziaji wa zahanati 8 na shilingi million mia tatu kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba vituo vipya vya afya.

 

 

Comments