Wanafunzi 13,358 Wa Shule Za Msingi Wilayani Kalambo Waripoti Shule Na Kuendelea Na Masomo.


Jumla ya wanafunzi 7563 wa madarasa ya awali wilayani Kalambo mkoani Rukwa kati yao wavulana wakiwa 3687 na wasichana 3906 wameripoti shule na wanafunzi 9765 kati yao wavulana wakiwa 4830 na wasichana 4935 wa darasa la kwanza wameripoti shule na kuendelea na masomo.

Hata hivyo kupitia ripoti iliotolewa na mkuu wa wilaya ya Kalambo kwenye vyombo vya habari Januari 14/2024 imeeleza kuwa Jumla ya wanafunzi 6389 waliandikishwa na kujiunga na elimu ya awali kati yao wavulana walikuwa 3125 na wasichana 3289.

Aidha kwa upande wa shule za sekondari jumla ya wanafunzi 4,887 walichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari kati yao wavulana wakiwa 2,319 na wasichana 2,568.

Comments