wakazi wa vijiji vya Kansapa na king’ombe wialaya ya Nkasi mkoani Rukwa wameondokana na matumizi ya mishumaa na vibatari kutokana na serikali kuwakamilishia mradi mkubwa wa umeme unao tajwa kuwawezesha kupunguza gharama za matumizi ya mafuta wakati wa uendeshaji viwanda vidogo vidogo.
Wameyasema
hayo kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani humo,ambapo wamesema awali
walikuwa wakilazimika kutumia vibatari na mishumaa na kwamba tangu kufikiwa na huduma hiyo kuwafikia wamefanikiwa
kuanzisha viwanda vidogo ikiwemo mashine za kusaga na kukoboa na kujikwamua
kiuchumi.
licha
ya hilo wameiomba serikali kutafuta ufumbuzi wa kudumu utakao saidia kuondoa
changamoto ya kukatika kwa umeme.
Mapema
akiongea na wakazi wa vijiji hivyo mkuu wa wilaya ya Nkasi Peter Lijualikali
amesema licha ya hilo serikali imetoa fedha million 500 ili kujenga zahanati
kutokana na vijiji hivyo kuwa na ukosefu wa huduma ya afya tangu kuanzishwa
kwake.
Comments
Post a Comment