Shule Ya Matai B Yagawanywa Kupunguza Msongamano Wa Wanafunzi.


Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kupitia idara ya elimu imeigawanya shule ya msingi Matai B na kuwa shule mbili tofauti kutokana kuwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi hatua itakayosaidia kurahisisha ufanisi wa kazi kwa walimu na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.

Shule hiyo ilikuwa na wanafunzi 3372 na walimu 32 ambapo kati ya hao wanafunzi 1200 na walimu 16 wamehamishiwa katika shule mpya ya Namlangwa ambayo ujenzi wake umekamilika.


Hata hivyo serikali ilitoa fedha million mia sita thelathini na nane na laki tano (638,500,000) kwa ajili ya ujenzi wa majengo 14 ikiwemo vyumba 2 vya madarasa vya wanafunzi wa awali na nyumba moja ya mwalimu ambayo imekamilika.


Comments