Madaraja 7 Yamesombwa Na Maji Na Nyumba 25 Kuanguka Katika Bonde La Ziwa Rukwa


 Madaraja saba na nyumba 25 zimebomoka katika vijiji 5 vya kata za Mtowisa Bonde la Ziwa Rukwa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa Nyakia chirukile akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, amewatembelea wathirika wa maafa hayo na kusema licha ya hilo mvua hiyo imeharibu mimea ya mazao mashambani ikiwemo mimea ya mahindi na mpunga hekali 1200 na kujitokeza kifo cha mtoto Wipnes Frank miaka 7 kujitokeza baada ya kugongwa na gogo.

 Aidha amesema mawasilino ya barabara inayo unganisha mkoa wa Rukwa , katavi na Songwe yamekatika na kuwataka wananchi kuacha kulima maeneo ya milimani ili kuepuka matukio hayo kujirudia.


Comments