Mahakama Ya Wilaya Ya Kalambo Yafanikiwa Kusajili Mashauri 216 Kwa Mwaka 2022

 


Mahakama ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kwa mwaka 2022 imefanikiwa kusajiri mashauri 216 na kumaliza mashauri 184 huku mashauri  32 yakishindwa kumalizwa kutokana na changamoto mbalimbali

Hakimu mfawidhi  mkazi wa Mahakam ya wilaya ya kalambo  kupitia kilele cha madhimisho ya siku ya sheria, Nikson Tem, amesema kwa mwaka  jana Mahakama zilifanikiwa kusajiri mashauri 375 na kumaliza mashauri 367 na kubakiza mashauri 8 na kwamba idadi hiyo ni pamoja na Mahakama za mwanzo

‘’maadhimisho ya siku ya sheria nchini huambatana na kauli mbiu au maudhui na kwamaka huu kauli mbiu yeu ni umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu ;wajibu wa mahakama  na wadau’’  alisema Tem

Alisema kauli mbiu hiyo imebeba ujumbe mahususi kuhusu wajibu wa mahakama na wadau wake katika kutumia njia ya usuruhishi katika kutatua migogoro kwa lengo la kukuza uchumi endelevu

Mapema kiongea kupitia maadhimisho hayo wakili wa serikali  Marietha  Maguta , aliwakikishia wananchi  na wadau wa sheria kuwa ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali  itaendelea kusimamia  kwa karibu maelekezo  yaliotolewa na kutoa kipaumbele chs kumaliza migogoro kwa njia ya maridhiano

‘’msisitizo wa ut


atuzi wa migogoro kwa njia ya mbadara na uikilizwaji wa mashauri kwa njia ya za kimahakama kama ulivyowekewa msingi imara kwenye sheria zetu unahitaji kuwekwa mazingira rafiki ,jambo ambalo pia limekuwa likihimizwa sehemu mbalimbali duniani’’ alisema Malietha

Kwa upande wake Deogratus Sanga , alisema  TLC imejiwekea mkakati wa kuanzisha kituo cha cha kimataifa cha usuluhishi wa migogoro kwa kushirikina na wizara ya katiba na sheria ambacho kitaiweka Tanzania katika ramani ya Afrika na dunia kwa kutekeleza dhana ya kutatua migogoro ya kibiashara za kimataifa nay a wawekezaji kwa njia ya suluhu

Hata hivyo, Tanzania ni muhimili ulioanzshwa na katiba ya Jamhuri ya mungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inatoa mamlaka kwa mahakama kuwa chombo cha kutoa haki kwa wakati na kwa wananachi wote

 

 

Comments