Dc Kalambo Asisitiza Viongozi Wa Serikali Kusimamia Kampeni Ya Upandaji Miti

 


Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Lazoro Komba  amewataka  watendaji wa serikali kusimamia zoezi la upadaji miti  kwenye maeneo yao husika kwa kudhibiti ukataji miti kiholea na upitishaji mifugo kwenye vyanzo vyamaji

Ametoa kauli hiyo wakati akizindua kampeni ya mkoa  ya  kupanda miti kwenye barabara  na makazi ya watu katika maeneo ya Utengule na Nambogo Manispaa ya Sumbawanga leo (Februari 08,2023)

Katika kuhakikisha kampeni ya urejeshaji uoto wa asili mkoani Rukwa inafanikwa mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amezitaka  halmashauri za Nkasi, Manispaa ya Sumbawanga, Kalambo na Sumbawanga kuboresha sheria ndogo ili ziweze kuchua hatua kwa waharibifu wa vyanzo vya maji


“Maafisa watendaji wa kata zote  jukumu lenu ni kwenda kusimamia zoezi la upandaji miti kwenye maeneo yenu. Maafisa Tarafa nendeni pia mkasimamie zoezi hili la upandaji miti Rukwa” alisisitiza Sendiga.

Sendiga alisema mkoa huo una changamoto ya utapiamlo ,hivyo sasa ni wakati wa wananchi kupanda miti ikiwemo ya matunda ili kuimarisha lishe ya familia.

Katika hatua nyingine Sendiga ametoa siku saba kwa Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Jane Nyamsenda kuhakikisha mitaa ya Manispaa ya Sumbawanga inakuwa safi pamoja na kupandwa miti na maua.


Kwa upande Mwenyekiti wa CCM Rukwa Silafu Maufi aliyeshiriki zoezi hilo alisema zoezi hilo la upandaji miti lililofanywa na viongozi wa Rukwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwa linapaswa kuwa endelevu.

“Nyumba zote za barabarani zipande miti kuanzia Sumbawanga hadi Tunduma ili kupendezesha mazingira. Miti ni pambo. Vipara vyote juu ya ardhi tuvipande miti” alisema Maufi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Jane Nyamsenda alisema programu ya upandaji miti iliyozinduliwa itakuwa utamaduni kwa wananchi wa Sumbawanga na kuwa itasaidia kurejesha uoto wa asili unaopotea kwa kasi.

 

 

Comments