Wilaya Ya Kalambo Mkoani Rukwa Yaadhimisha Wiki Ya Sheria Kwa Kufanya Matembezi


Kalambo- Rukwa

Wananchi Mkoani Rukwa Wameshauriwa kutatua migogoro Kwa Njia ya ustaarabu,amani , mazungumzo na Upatanishi ili kurudisha Mahusiano ya Kirafiki ambayo yatasaidia  Katika Upatikanaji wa haki bila kufungwa na masharti ya kisheria  ukilinganisha na njia ya uendeshaji wa Mashauri  kwa njia ya mahakama ambayo imekuwa ikichukua Muda Mrefu


Hayo yamesemwa  na mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Tano Mwela  Januari 22/2023 wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo kwa ngazi ya wilaya yamefanyika kwa kufanya matembezi kutoka eneo la Santamaria hadi katika ofisi za Mahakama ya wilaya hiyo


Amesema utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi ni takwa la katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ,ambapo utekelezaji wake ni muhimu ili kuendana na kasi  ya shughuli za ukuaji wa uchumi wa wananchi

‘’hivyo njia mbadala ya utatuzi wa migogoro inajumuisha utaratibu wa usuluhishi ,upatanishi,kurudisha mahusiano ya kirafiki na mazungumzo kufikia makubaliano ‘’ alisema Mwela

Alisema licha ya  hilo mahakama inawajibu wa kuongoza waadawa  katika kufikia makubaliano ,kuandaa wataalamu wa usuluhishi ikiwemo majaji na mahakimu kwa kuwaongezea ujuzi kwa njia ya mafunzo ,pamoja na kuweka mazingira rafiki ya usuluhishi na kutoa elimu kwa umma

Mapema akiongea  na hadhara ya wananchi katuka maeneo hayo  hakimu mfawidhi mkazi wa mahakama ya wilaya ya Kalambo, Nikison Tem , amesema  utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi una faida nyingi ikiwemo  upatikanaji haki kwa wakati na kwa gharama nafuu

Hata hivyo maadhimisho ya uzinduzi wa wiki ya sheria  unafanyika katika maeneo mbalimbali ambapo kwa ngazi ya kanda umefanyika katika mahakama kuu kanda ya sumbawanga mkoani Rukwa  na kuzinduliwa na jaji mkuu kanda ya Sumbawanga Dastan Ndunguru,

Comments