Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Tano Mwela amewataka wananchi wilayani humo kujenga mazoea ya kutunza miundombinu ya maji ili iweze kudumu na kuwa endelevu kutokana na serikali kutumia fedha nyingi katika kuiboresha na kuijenga
Aliyasema hayo wakati wa ziara ya
kamati ya usalama ya wilaya hiyo wakati
wa ukaguzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Mpombwe unaotekelezwa na wataalamu
wa ndani (Force Account ) kwa gharama ya shilingi milion 304,729,750.00 na
kusema mradi huo umejengwa kupitia ufadhili wa fedha za Benk ya Dunia
kupitia program ya PforR na kwamba utahudumia wakazi wapatao 3,058 na kudumu
kwa miaka 20.
Aidha aliwataka wananchi kuwa
walinzi kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka
husika dhidi ya mtu au watu wanaoharibu miundombinu ya maji ili waweze
kuchukuliwa hatua za kisheria
Mapema akiongea kupitia ziara hiyo Kaimu meneja wa Ruwasa wilayani humo Francis Mapunda , alisema katika kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu kimeundwa chombo cha watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO) kijulikanacho kwa jina la KAPOMBWE ambacho kitasimamia shughuli za uendeshaji na matengenezo ya miradi ya vijiji vya kata ya Kisumba na Mpombwe
Baadhi ya wananachi kijiji hapo
waliipongeza serikali kwa kukamilisha mradi huo na kwamba utawawezesha
kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu wakati wa kutafuta huduma ya maji
maeneo ya mbali
Comments
Post a Comment