Na IO – Kalambo.
Halmashauri ya wilaya ya Kalambo
mkoani Rukwa imeanzisha kampeni ya kusaka vipaji vya vijana kupitia Sanaa na
utamaduni kwa kupita mtaa kwa mtaa ili kuzindua matamasha ya ngoma za asili kwa
lengo la kupata vikundi ambayo vitashindanishwa katika mashindano ya wilaya.
Mapema
akiongea kupitia uzinduzi wa tamasha la ngoma za asili lililofanyika katika
kijiji cha mkowe wilayani humo afisa utamaduni wilayani humo Evance Showo
amesema Tamasha
la LINGOMA FESTIVAL 2022 limeasisiwa
na Ofisi ya Utamaduni na kuhusisha vikundi vinne(4) vya ngoma za Asili
vilivyopo katika kijiji cha Mkowe kwa malengo ya kuunga Mkono Juhudi za Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Katika kuboresha Sanaa na Utamaduni Katika
nchi yetu.
Alisema licha ya hilo Tamasha limebeba Ujumbe wa “UTAMADUNI WETU FAHARI YETU” na limelenga kutoa burudani kwa jamii na kujenga Mahusiano ya vikundi vya Sanaa na Utamaduni Vilivyopo Katika Jamii.
Awali wakiongea kupitia uzindunzi huo wananchi katika
maeneo hayo ambao licha ya kuipongeza serikali kwa kuanzisha Tamasha hilo
wakaitaka kuweka utaratibu maalumu ambao utasaidia vikundi hivyo kutambuliwa
ili viwe na uwezo wa kukopesheka kupitia taasisi za kifedha.
Comments
Post a Comment