Mwandishi Wa Kituo Cha ITV Na Radio One Mkoani Rukwa Apata Hati Ya Pongezi Kwa Kuandika Habari Za Michezo Ya Watoto Chini Ya Miaka 8 Kwa Kipind Cha Miaka 2 Mfululizo.
Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV na Radio one mkoani Rukwa Baraka Lusajo kwa mara nyingine amepata hati ya pongezi pamoja na zawadi kutoka kwa walimu wa michezo na maafisa michezo kutoka mikoa ya Rukwa Katavi na Songwe baada ya kuonesha uzalendo wa hali ya juu na kujitoa kwa moyo wake wote katika kazi yake ya uandishi wa habari akiandika habari mbalimbali za kijamii ikiwemo kukuza vipaji vya watoto wa shule za msingi kuanzia ngazi ya awali.
Mwandishi
huyo amepatiwa hati hiyo kutokana na kuandika habari za watoto katika kipengele
cha michezo na zilizo wezesha kuongeza ali ya ujifunzaji darasani.
Kaimu
afisa michezo mkoani Rukwa Amos Mmewa, alibainisha kuwa uwepo wa michezo kwa
watoto imekuwa ikisadia kuongeza ali ya uelewa darasani kwa watoto na kwamba
mpaka sasa wameweka mkakati wa kutoa elimu kwa waalimu wa michezo kutoka mikoa
mitatu ikiwemo Rukwa, Katavi na Songwe lengo likiwa ni kuhakikisha watoto wa
awali wanapewa kipaumbele katika michezo.
‘’walimu
hawa wa michezo wanaenda kuwa msaada mashuleni katika kuendeleza vipaji vya
watoto kwa kubuni michezo mbalimbali ambayo inaenda kusaidia katika swala la
makuzi na maendeleo ya watoto kiakili’’ alisema mmewa.
Kwa
upande wake mkufunzi kutoka chuo cha michezo cha Malya Erick Mfugale, alisema michezo
hiyo inalenga watoto wenye umri kuanzia
miaka 3 na kwamba lengo likiwa ni
kuongeza kiwango cha ulewa darasani.
Alisema
Tanzania ni nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki katika kutoa elimu
ya awali na kuifanya kuwa ya lazima kwenye sera ya elimu na mafunzo ya ufundi na
kwamba kwa kutambua hilo wadau wa michezo wameona kuna umuhimu wa kutoa elimu
kwa maafisa michezo na walimu wa michezo ili kuwajengea uwezo zaidi juu ya
umuhimu wa michezo kwa wanafunzi wa awali.
‘’vilevile
mtaala wa elimu ya awali unasaidia ujifunzaji kupitia michezo na mwongozo wa
serikali wa mwaka 2016 wa elimu bila malipo hujumuisha elimu ya awali .Aidha
uandikishwaji wa elimu ya awali ni
kiashiria muhimu kilicho ingizwa katika
mpango wa kitaifa wa maendeleo ya miaka
mitano 2016/17-2020/21.
Comments
Post a Comment