Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Tano Mwela amemuagiza mganga mkuu wa wilaya hiyo kuhakikisha zoezi la utoaji chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano linafanyika kwa weredi na kwa ustadi mkubwa na kusisitiza kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watumishi ambao watabainika kuandika data za uongo wakati wa uendeshwaji wa zoezi hilo.
Ugonjwa
wa polio ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya polio ambapo kwa mara ya
mwisho Tanzania ilipata mgonjwa wa polio Julai 1996 na kuja kugundulika tena Februal
2022 katika nchi jirani ya Malawi ambako mgonjwa wa kwanza alipatikana katika
mji mkuu wa Malawi.
Hata hivyo tathimini iliyofanywa na wizara Afya kwa ushirikiano na shirika la afya Duniani {WHO} nchi ya Tanzania ilionekana kuwa miongoni mwa nchi zilizo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa polio endapo kama hatua madhubuti hazitochukuliwa kwa haraka.
Awali
akiongea wakati wa kikao ch a mafunzo kwa kamati ya msingi ya Afya ngazi ya
jamii {PHC} Mganga mkuu wilayani humo Dkt Eugen Lutaisire,alisema zoezi hilo
litafanyika nyumba kwa nyumba na mtoto kwa mtoto.
‘’Sambamba
na uchanjaji huduma zingine zitatolewa ikiwemo elimu ya chanjo,kuimarisha
huduma za chanjo katika vituo vya kutolea chanjo ikiwemo kuwatafuta na kuwafuatilia watoto
wote wenye umri chini ya miaka miatano 5, ambao wamepata ulemavu wa ghafla tepetepe {washukiwa wa ugonjwa wa polio} na
kutoa taarifa katika vituo vilivyopo karibu kwa uchunguzi na kubaini ugonjwa huu
wa polio’’ alisema DkT Eugen.
Alisema
ugonjwa wa Polio unasababishwa na Virusi vya polio na husababisha kupooza na
hatimaye kifo na kusisitiza kuwa virusi vya polio huingia mwilini kwa njia ya
mdomo , kwa kunywa maji au chakula ambacho kimechafuliwa na kinyesi.
Awali
akifungua kikao cha PHC wilayani humo mkuu wa wilaya ya Kalambo Tano Mwela,alisema
hata sita kuchukua hatua dhidi ya watumishi ambao watabainika kutoa data za uongo wakati wa uendeshwaji wa
zoezi hilo na kusisitiza taarifa zote
kuwekwa kwa maandishi na kwa kufuata utaratibu.
‘’Taarifa
zote ziwe kwa maandishi na zoezi hili nitafuatilia kwa ukaribu hivyo nataka
zoezi hili lifanyike kwa weredi mkubwa’Alisistiza Mwela.
Comments
Post a Comment