Mkuu wa Mkoa wa Rukwa
Mhe. Joseph Mkirikiti ametoa taarifa ya Mkoa wa Rukwa katika kipindi cha mwaka
mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uwepo wa amani na utulivu, umoja na mshikamano
ambapo wananchi wa Mkoa wa Rukwa wamekuwa wakiendelea kufanya shughuli zao za
kujiongezea kipato bila vikwazo vyovyote.
Akizungumza ofisini kwake
Mkirikiti ametoa ufafanuzi katika miradi mbalimbali iliyotolewa fedha na
serikali na mafanikio yaliyopatina ambapo Sekta ya Afya Katika kipindi cha
mwaka mmoja mkoa umepokea shilingi Bilioni 1.3 kwaajili ya ujenzi wa vituo vya
afya vitano (05) .
Sekta ya maji Mkoa
umepata mafanikio makubwa katika sekta ya maji ambapo jumla ya Miradi 99 yenye
thamani ya shilingi Bilioni 25.5 ilisainiwa kwa ajili ya kuanza utekelezaji
ambapo kati ya hizo shilingi Bilioni 16.6 zilipokelewa kwa ajili ya utekelezaji
wa Miradi hiyo ya maji na tayari miradi 39 imekamilika na inatoa maji.
Kwa upande wa Sekta
ya Elimu katika kipindi cha mwaka mmoja tumepokea jumla ya shilingi Bilioni
16.5 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya elimu ya Msingi,
Sekondari, Chuo cha ualimu Sumbawanga na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.
Katika kuhakikisha
kuwa Barabara zinapitika kwa ajili ya kuinua uchumi wa wananchi wa Mkoa wa
Rukwa, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kujidhatiti kuhakikisha kuwa
Barabara zilizopo chini ya TANROADs na TARURA zinatengenezwa na kupitika muda
wote
Mkoa umepangiwa
Shilingi Bilioni 15 kwa ajili ya maendeleo na matengenezo ya Barabara ambapo
hadi kufikia mwezi Machi tayari tumepokea jumla ya shilingi Bilioni 12.4 kwa
ajili ya matengenezo na maendeleo ya Barabara zilizo chini ya Wakala ya
Barabara Tanzania
Comments
Post a Comment