Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Tano Mwela
amesema maandalizi kwa ajili ya ziara ya kutembelea kivutio cha utalii cha maporomoko ya maji ya Kalambo yamekamilika na kuwa sasa yatafanyika tarehe 18 Desemba mwaka huu lengo ikiwa kukuza utalii wa ndani ya Mkoa wa Rukwa .
Mwela ametoa taarifa hiyo leo mjini Sumbawanga alipoongea na
wanahabari na kubainisha kuwa
‘’Ikumbukwe Kalambo water
Falls Ni Mapolomoko ya Pili kwa ukubwa kutoka Yale ya Afrika kusini.Pia ina
vivutio vya misitu ya Asili,Hifadhi na Maeneo ambayo yanavutia kiutalii.Yapo maeneo
ya kuweka makambi kwa ajili ya kuchoma Nyama,ngoma,Kuogelea, Jogging na
Burudani mbalimbali huku ukilitazama jua la kuzama kwa uzuri(Sun set) kupitia
ziwa Tanganyika,ziwa lililojaa Samaki wenye Radha ya kipekee barani Afrika.Maji
yake meupe yenye kukuwezesha kuona kina kwa chini na kukupa urahisi
Kuogelea.Tembelea maeneo hayo usiishie tu kusimuliwa’’ alisema Mwela.
Comments
Post a Comment