DC NAWANDA AFUNGUA SEMINA YA MAFUNZO KWA WADAU WA USAFIRISHAJI MKOANI TABORA



Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini, Yahaya Nawanda, akifungua Semina ya mafunzo kwa wadau wa usafirishaji (hawapo pichani), kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, mkoani Tabora.

             


Mhandisi Joseph Rwihura, ambae ni Mhandisi Mkuu Matengenezo ya Mizani kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), akitoa elimu kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018 kwa wadau wa usafirishaji mkoani Tabora



Baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo kuhusu Sheria ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Afrika Mashariki ya mwaka 2016 na kanuni zake za mwaka 2018, wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo mkoani Tabora

Comments