Wananchi
kutoka vijiji 16 vinavyozunguka Maporomoko ya maji ya mto Kalambo wameanza
kunufaika na uwepo wa Maporomoko hayo baada ya Serikali kuanza kufanya
maboresho ya miundombinu ya barabara itakayogharimu zaidi fedha kiasi cha Shilingi
milioni 132 za Kitanzania
Msitu
wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Kalambo una ukubwa wa hekta 43,334 na unamilikiwa
na kusimamiwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kupitia kanda ya
nyanda za juu kusini wilaya ya Kalambo.
Hifadhi
hiyo ilihifadhiwa kisheria mwaka 1957 na ilipandishwa hadhi kuwa hifadhi ya
mazingira Asilia mwaka 2019 baada ya kuonekana kuwa na hazina kubwa na Hifadhi
hii ilihifadhiwa kisheria mwaka 1957 na kupandishwa hadhi kuwa Msitu wa
kutangazwa na gazeti la serikali mwaka 2019 chini ya usimamizi wa Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS) ukiwa na ukubwa wa hekta 43,334.
Licha
ya uwepo wa msitu huo lakini pia kuna kivutio kikubwa cha Maporomoko ya maji ya
Kalambo yenye umaarufu katika bara la Afrika na duniani kote. Umaarufu wa
maporomoko hayo umerekodiwa katika maandiko mbalimbali.
Maporomoko
hayo yanapatikana katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Kalambo uliopo
wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania kwenye
latitude 08′3″ kusini na longitude 3 7′14″ Mashariki. Hifadhi ya Mazingira
Asilia ipo karibu sana na Ziwa Tanganyika katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa
takribani kilomita 20 kutoka maeneo husika.
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 1920 na kurekodiwa katika maandiko
mbalimbali (Wikipedia) ilionyesha kuwa maporomoko hayo yana urefu wa meta 235
na upana wa kati ya meta 3.6-18.
Pia
maporomoko hayo ni ya pili barani Afrika baada ya Maporomoko ya TUGELA yaliopo nchini Afrika kusini.
Maporomoko
hayo yapo umbali wa Km 120 kutoka Sumbawanga Mjini. Kuna njia kuu tatu za
usafiri ili kufikia maporomoko haya: Usafiri wa kutumia barabara: Kutoka Dar-es-Salaam-
Sumbawanga – Matai. kutoka Mwanza – Sumbawanga – Matai. Pia unaweza kutuimia
usafiri wa Ndege au usafiri wa maji kupitia ziwa Tanganyika
Aidha
wageni kutoka Arusha, Mwanza na Dar-es- Salaam wanaweza tumia Uwanja wa ndege
wa Songwe uliopo Mkoani Mbeya baada ya hapo kutumia barabara kutoka Mbeya hadi
Sumbawanga Usafiri wa kutumia njia ya majini: Watalii wanaweza tumia Meli toka
Manispaa Kigoma hadi bandari ya Kasanga iliyopo wilayani Kalambo
Pia
Mtalii atakapokuwa anashuka kuelekea kwenye maporomoko atapata fursa ya kupata
mwonekano (View points) vilivyopewa
hadhi ya majina ya viongozi muhimu Kituo cha kwanza; Proffesor Dossantos Silayo
View point (baada ya mita 299.6) Kituo cha Pili; Brigedia Jenerali Mkeremmy
View point (baada ya mita 239.9) Kituo cha tatu; Dr. Hamis Kigwangala View
point (baada ya mita 157.5).
Awali
akiongea wakati wa maadhimisho ya siku ya utalii dunia yalioenda sambamba na utoaji
zawadi za michezo katika kijiji cha mpombwe wilaya ya kalambo mkoani Rukwa ,mhifadhi
mkuu wa hifadhi ya mto Kalambo Joseph Chezue ,alisema michezo hiyo inalenga kutoa elimu kwa
wananchi juu ya umuhimu wa kutembelea na kulinda vivutio vya utalii.
Alisema
watoto ni kundi jingine ambalo linapaswa kupewa kipaumbele katika swala zima la
kulinda na kutunza vivutio vya utalii na
kusisitiza walimu kutoa fulsa kwa watoto wa shule kutembelea vivutio vya utalii
ikiwemo maporomoko ya kalambo fallse.
Comments
Post a Comment