Serikali ihamasishe upandaji miti mashuleni ili kuliwanda watoto na maafa.



Wananchi wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kulifanya zoezi la upandaji miti kuwa ajenda ya kudumu kwa kuhakikisha kila kaya inakuwa na miti ya kutosha ambayo itawezesha kuondokana na tatizo la maafa ambayo yamekuwa yakijitikeza na kusababisha baadhi ya watoto wa shule kupata shida kutokana majengo ya shule kuezuliwa na upepo kwa baadhi ya maeneo.

Wameyasema hayo kupitia maadhimisho ya maafa duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika kijiji cha Matai ‘’B’’ Wilayani humo na kusisistiza serikali   kusisitiza swala la upandaji miti kwenye maeneo ya taasisis ikiwemo shule ili kuwalinda watoto wa shule na majanga hayo.


 Awali akiongea kupitia maadhimisho hayo mkuu wa wilaya hiyo Tano Mwela ,alisema kwa halmshauri ya Kalambo mwaka 2020/2021 jumla ya kaya 245 zilipoteza makazi kutokana na maafa na kwa mwaka huo huo maafa yalisababisha vifo vya watu wawili.

Alisema katika kushughulikia changamoto hizo wilaya itahakikisha inawatumia wataalam wa ujenzi wa maendeleo ya jamii,watendaji wa vijiji katika kutoa elimu ya jinsi ya kufuata taratibu za ujenzi ili kuepuka maafa.

 

 

Comments