Watu 36 Wakiwemo Askari Watatu Wa SUMAJKT Wanashikiliwa Na Jeshi La Polisi Kwa Tuhuma Za Mauaji Na Uwizi Wa Pikipiki.
Jeshi
la polisi mkoani Rukwa limeripoti matukio matatu tofauti likiwemo la watu 36
wakiwemo askari watatu wa SUMA JKT ambao ni walinzi wa chuo cha udaktari cha Bakhita
wilayani Nkasi baada ya kuhusika na tuhuma za mauaji kwa kumpiga na lungu mtu
aliyedaiwa kuwa ni mwizi kisha kusababisha kifo chake hapo papo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo ACP William Mwampagale amesema katika tukio la kwanza wanawashikilia watu watano wakiwemo askari watatu wa SUMA JKT kwa tuhuma za kusababisha kifo cha mtu aliyedaiwa kuwa ni mwizi.
‘’Tulifanikiwa
kuwakamata watuhumiwa watano kati yao wakiwemo askari watatu wa SUMA JKT ambao
ni walinzi wa chuo cha taaluma ya udaktari wa tiba kiitwacho Bakhita kilichopo
wilaya ya Nkasi kwa kosa la kumpiga na kusababisha kifo cha mtuhumiwa ambaye
walimkamata kwa kosa la wizi. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani muda wowote
upelelezi utakapokamilika.’’alisema kamanda Mwampagale.
Alisema
katika tukio lingine wanawashikiria watu 31 wakiwa na pikipiki 21 ambazo
umiliki wake ni wa mashaka.
Alisema kati ya hao watuhu
miwa watatu wametiwa hatiani na kufungwa jela na watuhumiwa wengine watafikishwa mahakamani muda wowote pindi upelelezi utakapo kamilika
‘’Pia
katika tukio jingine tumefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sugu wa uvunjaji kwenye
mikoa ya jirani na hapa kwetu wakiwa na Kompyuta mpakato 2 aina ya Sumsung Chrome
na moja aina ya HP, Printer moja,Mashine ya kupigia mapigo ya moyo na begi
mbili ndogo vyote mali ya Jerone Longe raia wa Marekani’’alisema kamanda Mwampagale.
Licha
ya hilo aliwataka wananchi mkoani humo kuendelea kushirikiana na jeshi la
polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu ili kuzuia matukio ya uhalifu wa aina zote.
Comments
Post a Comment