Wanafunzi wawili watunukiwa medani na kombe baada ya kugundua dawa ya kuuwa wadudu kwenye mimea ya mahindi


Wanafunzi wawili wa shule ya Sekondari Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa wametunukiwa medani na kombe la ushindi baada ya kufanikiwa kugundua dawa ya kuua wadudu waharibifu kwenye mimea ya mahindi na maharage ambayo itawawezesha wakulima kuondokana na adha ya kuharibika kwa mazao yao mashambani wakati wa msimu wa kilimo

Awali akikabidhi zawadi hizo Afisa elimu sekondari wilayani humo Jeshi Lupembe, alisema wanafunzi hao waligundua dawa ya kuua wadudu kwenye mimea ya mahindi maharagwe pamoja na mboga mboga.

Alisema dawa hiyo ilipelekwa kwenye mashindano kitaifa ambapo wanafunzi hao waliibuka na ushindi wa pili kitaifa baada ya dawa hiyo kugundulika kufanya kazi vizuri na kupatiwa zawadi ya fedha shilingi millioni mbili, kombe pamoja na medani kama hamasa ya wanafunzi wengine kuyapenda masomo ya sayansi.

Wanafunzi hao kwa upande wao walisema kupatiwa Zawadi hizo itaongeza hamasa Zaidi ya watu wengine kuyapenda masomo ya sayansi.

Comments