Benard Mwamsojo Ashinda Kwa Kishindo Kura Za Maoni Ndani Ya Chama Kuwania Nafasi Ya Udiwani Kata Ya Lyowa.
Wajumbe wa chama cha Mapinduzi CCM kata ya Lyowa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wamempitisha Benard Mwamsojo kuwa mgombea wa kiti cha udiwani katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika kitaifa oktoba 9/2021 baada ya kupitishwa kwa kura 66 kati ya wagombea 13 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo.
Uchaguzi huo umejumuisha wagombea 13 na wajumbe 154 na kumchagua Benard Mwamsojo kwa kura 66 akifuatiwa na Meshack Sikonde aliepata kura 30,Crispin Nyau nyau kura 25, Tito Simwela kura 9, Derick Simtowe kura 7, Edigi Nkanga kura 3, Flibert Kachonta kura 3,Leonard Changala 3 , Leonard Mwanalinze 0, Sulumu Mosud kura 1, Nestory Kazuwi kura 2, Nicas Karolo kura 3.
Msimamizi
wa uchaguzi huo ambae pia ni mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Daud Sichone,
amesema uchaguzi huo ulikuwa wa wazi huru na haki huku wagombea wakiahidi kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa mshindi wa nafasi hiyo.
Uchaguzi huo unafanyika ili kuziba pengo la aliekuwa diwani wa kata hiyo Legius Boimanda aliefariki dunia hivi karibuni wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa mjini Sumbawanga.
Msimamizi
wa uchaguzi jimbo la Kalambo Shafi Kassm Mpenda ametangaza siku ya tarehe 9
oktoba 2021 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Lyowa na kwamba
mchakato wa uchaguzi utaanza rasm tarehe 13/ September 2021.
‘’
kwa mujibu wa mashariti ya kifungu cha 13 {1}
cha sheria ya uchaguzi ya serikali za mitaa sura ya 292 , waziri mwenye dhamana
na serikali za mitaa aliitaarifu tume ya uchaguzi uwepo wa nafasi wazi ya
udiwani katika kata ya Lyowa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo.’’ Alisema mpenda
kupitia Tangazo.
Comments
Post a Comment