Wadau wa soka wilayani Kalambo mkoani Rukwa wameungana na kuanzisha timu ya mpira wa miguu Wanawake inayofahamika kama NYOTA NJEMA QUEENS itakayoshiriki michuano mbalimbali ya ndani na nje ya mkoa huo huku lengo likiwa ni kuibua na kukuza vipaji vya wanawake kupitia michezo hiyo.
Hayo
yamebainishwa na mwenyekiti wa timu hiyo CHARLES SENGELE wakati wa kukiaga
kikosi hicho kuelekea mashindano ya timu za wanawake mkoani humo ambayo
yanayofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga, ambapo amesema
lengo la michezo hiyo ni kuhakikisha wanawake wanapewa kipaumbele.
Alisema baada ya wilaya hiyo kukosa timu kwa muda mrefu walilazimika kukaa kikao na kufanya uchambuzi wa wachezaji kisha kuweka kambi ya siku thelathini kwa ajili ya maandalizi ya ligi ya mkoa.
Alisisitiza
wadau kujitokeza kuidhamini timu hiyo kutokana na kuendeshwa kwa mfumo wa
michango ya wadau kutoka maeneo tofauti ya wilaya hiyo na kwamba kikosi hicho
kina wachezaji wapatao kumi na nane.
Comments
Post a Comment