Mwenge wa uhuru umetembelea na kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo wilayani Kalambo ikiwemo mradi wa ujenzi wa miundombinu
ya mradi wa maji Singiwe unaogharimu fedha kiasi cha shilingi million
265,263,744.07
Akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi huo meneja wa
RUWASA wilayani humo Patrick Ndimbo amesema mradi huo unatarajia kuhudumia wakazi
5,968 kutoka vijiji vya Singiwe na Charaminwe
Alisema katika kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu wilaya kupitia RUWASA imeunda na kusajili kikundi cha watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO) kilicho sajiliwa kwa jina la NZWALO ambacho kinasimamia shughuli za uendeshaji na matengenezo ya mradi huo
Awali akizindua mradi huo kiongozi wa mbio maalumu
za mwenge wa uhuru Luten Josephine Mwampashi,aliwataka wananchi kuendelea
kuulinda mradi huo ili uweze kudumu kwa
muda mrefu
Duh safi sana mkuu kwa kutufikishia taarifa moja kwa moja ndani ya wilaya yetu!
ReplyDelete