Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imefanikiwa kusajiri vikundi 31 vya wanawake vijana na wenye ulemavu kwa mwaka 2020/2021 huku jumla ya fedha tasilim shilingi million sitini ( 60,000,000/=) zikikopeshwa kwenye vikundi hivyo kwa lengo la kuvijengea uwezo kiuchumi na kupunguza umasikini wa kipato.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya Maendeleo ya jamii hivi karibuni kupitia
baraza la madiwani la robo ya nne ya mwaka 2020/2021 wilayani humo, ilielezwa
kuwa kazi zingine zilizofanyika ni pamoja na uhamasishaji jamii kwenye ujenzi wa
miradi ya maendeleo, kuratibu shughuli zinazofanywa na mashirika yasiyo kuwa ya
kiserikali, kunusuru kaya masikini kupitia
mpango wa TASAFU III unaotekelezwa katika vijiji 66 kupitia uhaulishaji fedha
kwa kaya masikini 4,312 ambapo jumla ya shilingi million 927,168,460 zilitolewa
hadi kufikiia juni 30/2021.
Hata
hivyo, kupitia zoezi la hivi karibuni la utambuzi na uandikishaji wa kaya
masikini katika vijiji 45 vilivyokuwa nje ya mpango huo, Halmashauri imepata
mafanikio makubwa ambapo jumla ya kaya 5,270 zilidodoswa kwa wawezeshaji
kutembea kaya kwa kaya kwa lengo la kuingiza taarifa muhimu zinazotakiwa kwenye
mpango,
Comments
Post a Comment