Halmashauri Ya Kalambo yafikia asilimiaa 82 ya ukusanyaji mapato Kwa Mwaka 2020/ 2021.


 Halmashauri Ya Kalambo  yafikia asilimiaa 82 ya ukusanyaji mapato Kwa Mwaka 2020/ 2021.

Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa hadi kufikia June 2021 imefanikiwa kukusanya fedha kiasi cha shilingi 1,516,756,756,500.00 sawa na asilimia 82 ya lengo lililokasimiwa la kukusanya shilingi billion 1,853,110,000 kwa mwaka 2020/2021.

Idara ya fedha ni miongoni mwa idara za Halmashauri hiyo ambayo inafanya kazi ya kusimamia mapato na matumizi ya fedha za umma ikiwemo ukusanyaji mapato ya ndani, kupokea fedha kutoka serikali kuu na kufanya malipo mbalimbali kadri ya miongozo na taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za manunuzi na huduma za jamii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya mipango kupitia baraza la madiwani   wilayani humo, ilielezwa kuwa hadi kufikia Juni 2021 kiasi cha shilingi 1,377,093,744.28 kilitumika sawa na asilimia 74.31 ya bajeti iliyotengwa na kwamba fedha hizo zilitumika katika miradi ya maendeleo.

 Hata hivyo kupitia baraza hilo madiwani waliazimia kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji na kata ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wataalamu katika kubuni vyanzo vipya vya mapato.

 


Comments