Mahakama ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imemhukumu Ibrahimu moses mkazi wa kijiji cha Kisumba mwenye umri wa Miaka 26 kutumikia kifungo cha miaka 31 jela kwa kosa la kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15.
Akisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya wilaya hiyo NCKSON TEMU, mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Rajabu Ndunda amesema mshitakiwa alishitakiwa kwa kosa la kubaka na kumshambulia mwanafunzi kinyume cha sheria na kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo machi 9,2020 kwa kumwingilia kimwili bila ridhaa yake. Wakati wa ungamo,mshitakiwa aliiomba mahakama
isimpe adhabu kali kwani hilo ni kosa lake la kwanza na pia anafamilia
inamtegemea .yenye mke na mtoto mmoja.
Mwendesha mashitaka hakuwa na kumbukumbu za nyuma za mshitakiwa na aliiomba mahakama impe adhabu kali mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia chafu na ovu kama hiyo.
Awali, akisoma hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya wilaya hiyo Nikison Tem , amesema mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na sheria kifungu cha 130 na (2)(e) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 mapitio ya mwaka 2019 pamoja na kifungu cha shambulio la kudhuru mwili kifungu cha 241 cha kanuni ya adhabu sura na ya 16 ya mapitio sheria ya mwaka 2019.
Aidha kwa kuzingatia utetezi
wa mshitakiwa na maombi ya Mwendesha mashitaka,Hakimu alimhukumu mshitakiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka huku
kosa la kushambulia mwili akihukumiwa mwaka mmoja na kufanya jumla ya miaka 31.
Comments
Post a Comment