Watoto wa shule wahimizwa kutunza mazingira

Na Baraka Lusajo - Rukwa 


Shirika linalo husika na utetezi wa mzingira nchini LEAT limeadhimisha siku ya mazingira dunia kwa kuendesha michezo pamoja na kukabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa watoto wa shule za msingi katika bonde la ziwa Rukwa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Siku hii inayoadhimishwa ulimwenguni kila mwaka na ilianza zaidi miaka 40 iliyopita na huvuma Zaidi kwenye mitandao ya kijamii.

 Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yamepanuka na kuwa jukwaa la kimataifa la kuhamasisha na kuchukua hatua kuhusu masuala nyeti ya mazingira kuanzia kwa uchafuzi baharini, ongezeko lajoto duniani hadi kwa matumizi ya bidhaa kwa njia endelevu na uhalifu dhidi ya wanyamapori. 

Hata hivyo Mamilioni ya watu wameshiriki katika miaka iliyopita, na kuleta mabadiliko jinsi tunavyotumia bidhaa na kwenye sera za mazingira za kitaifa na kimataifa.

Tangu mwaka wa 1974, imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tarehe 5 mwezi wa Juni ikileta pamoja serikali, mashirika ya biashara na wananchi kushughulikia masuala nyeti yanayoathiri mazingira.

 Hata hivyo kwa mkoa wa Rukwa maadhimisho hayo yaliadhimishwa kwa njia tofauti tofauti, ambapo katika bonde la ziwa Rukwa shirika la LEAT  liliadhimisha maadhimisho hayo kwa  kutoa elimu kwa wananchi pamoja na  kugawa vifaa vya michezo kwa watoto wa shule.

Mkurugezni wa shirika hilo Kelvini Swai alisema Siku ya Mazingira Duniani ni jukwa la kimataifa la kuleta mabadiliko chanya. Huhimiza watu binafsi kutafakari kuhusu kile wanachokila kwa mashirika ya biashara kubuni mifumo isiyochafua mazingira kwa wakulima na makampuni

Alisema siku hiyo huzingatia Zaidi uzalishaji kuzalisha kwa njia endelevu kwa serikali kuwekeza kwenye uboreshaji wa mazingira kwa taasisi za elimu kuelimisha wanafunzi kuchukua hatua na kwa vijana kujenga hatima isiyochafua mazingira.

Alisema shirika hilo lina hakikisha watoto wanakuwa msitari wa mbele katika kuboresha mazingira yao.

Hata hivyo katika wilaya ya Kalambo maadhimisho hayo yaliadhimishwa kwa kutoa elimu kwa wafugaji kuhakikisha wanatoa lishe ya maziwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 .

Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Wilbroad Kansapab, alisema wafugaji wanawajibu wa kutunza mazingira kwa kuacha kupitisha mifugo kwenye vyanzo vya maji pamoja na kuto kata miti hovyo.

Alisema wagaji wanawajibu wa kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule badara ya  kuwapeleka machungoni.

 

Comments