Watano Wanaswa Na Siraha Aina Ya Pisto Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa.

Jeshi la Polisi la mkoani Rukwa linawashikilia watu watano kwa kujihusisha na matukio ya kiuharifu ikiwemo matumizi ya siraha kinyume na utaratubu.

Katika operesheni iliofanyika wilayani Kalambo Jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata mtu mmoja baada ya kupatikana na siraha moja aina ya Pisto iliokuwa imetengenezwa kienyeji na kwamba siraha hiyo ilikuwa ikitumika katika shughuli za uwindaji haramu.

Hata hivyo katika Operesheni hiyo Jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata mtu mmoja huko katika eneo la Reginamundi lililopo kata ya Izia Tarafa ya Lwiche manispaa ya Sumbawanga akiwa na kete 3 za Bhangi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa Kamishna Msaidizi wa polisi Wiliam Mwampagale,alisema licha ya hilo katika Manispaa hiyo walifanikiwa kumkamata mtu mmoja akiwa  na noti mbili za bandia .

Mbali na hilo Kamanda Mwampagale alisisitiza kuwa Jeshi hilo limeendelea na Operesheni hiyo maalumu   na kufanya ukaguzi wa Magari 915 ambayo kati ya hayo Magari 574 yalionekana kuwa ni mazima, magari 333 yalionekana ni mabovu  na jumla ya magari 8 yaliondolewa namba  kwa kukosa sifa za kutembea barabarani.

‘’jumla ya madereva 732 walichukuliwa hatua mbalimbali za kisheria ikiwa ni pamoja na kutozwa faini na kiasi cha shilingi 21,960,000/= kilikusanywa kutokana na makosa hayo.

 


Comments