Na Baraka Lusajo - Rukwa
JAMII
Mkoani Rukwa imetakiwa kuendelea kupinga na kukemea
matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto kutokana na makosa hayo wilayani
kalambo kuongezeka kutoka matukio 27 kwa mwaka 2020 hadi kufikia makosa 37 kwa
mwaka 2021 sawa na asilimia 0.45 huku watu 12 katika kipindi cha miezi mitano
wakihukumiwa kifungo cha maisha jela kutokana na tuhuma za ubakaji wa watoto.
Akiongea kupitia maadhimisho ya
mtoto wa Afrika ambayo Kimkoa yamefanyikia wilayani Kalambo mkoani Rukwa mratibu wa dawati la jinsia na watoto wilayani humo Anna Kimbe, Alisema
“Kwa
kipindi cha miezi mitano mwaka 2021 ambapo jumla ya makosa 32 yaliyo ripotiwa
ukilinganisha na miezi mitano mwaka 2020 ambapo makosa yaliyoripotiwa hii ni
sawa na ongozeko la makosa 5 ambayo ni sawa na silimia 0.45’’. Alisema Kimbe
Alisema makosa ya ukatili wa kijinsia yaliongezeka baada ya elimu kutolewa na kusababisha jamii kutambua umihimu wa kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola.
‘’Makosa
ya ukatili yameongezeka baada ya elimu kutolewa kwa jamii hivyo jamii kutambua
umuhimu wa kutoa taarifa za malalamiko hayo kituo cha polisi kwa wakati tofauti
na kipindi cha nyuma kabla ya elimu kuifikia jamii,ambapo hata walipotendewa
ukatili walimaliza majumbani kwao, alisema Kimbe.
Mkuu
wa wilaya hiyo kalorius misungwi ambae alikuwa ni mgeni Rasmi kwenye
maadhimisho hayo alisema wananchi wanawajibu wa kuendelea kuwalinda watoto
dhidi ya matukio ya ukatili.
Comments
Post a Comment