Michezo Ya Umitashumta Yatajwa Kuibu Vipayji Vya Watoto

Na Baraka Lusajo - Rukwa

Serikali mkoani Rukwa imeanza harakati za kuunda timu moja itakayo shiriki katika mashindano ya umitashumta ambayo kitaifa inatarajiwa kufanyika Juni 2021 mkoani Mtwara huku wanafunzi wakitakiwa kuitumia michezo hiyo katika kuimarisha afya na kuibua vipaji vyao.

Michezo hiyo inatarajiwa kuanza kufanyika mkoani
mtwara kuanzia Juni 6 hadi 19 /2021, ambapo wachezaji kutoka Halmashauri 4 za Mkoa wa Rukwa.

Hata hivyo wanafunzi wapatao 400 wanashiriki kwenye michezo hiyo ambayo inafanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Matai.

Uanzishwaji wa michezo ya UMITASHUMTA ulikuwa na lengo la kuibua, kuvitambua na kuviendeleza vipaji mbalimbali vya wanafunzi wangali wapo shuleni kwa madhumini kuwajengea Ari, uthubutu na hamasa ili kuwakuza na kuwaimarisha na kuwajengea misingi thabiti ya kimichezo.


Awali akiongea kupitia uzinduzi wa michezo hiyo mkuu wa wilaya ya Kalambo Kalorius Misungwi, alisema mashindano hayo yana umhimu mkubwa katika kuibua, kutambua na kuendeleza vipaji mbalimbali vya watoto.

“Nitumie fursa hii kuwatakia maandalizi mema katika kuendesha mashindano na kuwaandaa vijana na michezo kwa mashindano ya taifa. ni imani yangu kuwa mtauwakilisha Mkoa wetu vizuri kwa kufanya vizuri kwenye mashindano ya taifa.’’alisema Misugwi.


Aidha alisema kupitia michezo hiyo imesaidia kuibua wanamichezo mahiri nchini wakiwemo akina Juma kaseja, Jarson Tegete, Juma Abdul Telela, Renatus Njohole.

“Kwa muktadha huo niwaase tu wasimamie na kuhakikisha vijana hawa wanafikia ndoto zao. Tuangalie mifano ya wanamichezo na wasanii waliofanikiwa kama Mbwana Samatta na msanii Nasibu Abdul Maarufu kama Diamond Platnum ambao kupitia vipaji vyao wanapata fedha nyingi na wameajiri watu wengi. Hivyo tusichukulie kawaida vipaji vya watoto hawa kwa kuwa vinaweza kubadilisha maisha yao na kuchangia uchumi wa Taifa letu”. Alisema Misungwi

Hata hivyo michezo hiyo ni maandalizi ya kushiriki mishindano ya umitashumta ambayo inashirikisha  shule zote nchini, ambapo kwa  mwaka 2021 michezo hiyo inatarajiwa kufanyika mkoani Mtwala.

Comments