Na Baraka lusajo - Rukwa
Katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani nchini Tanzania Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema licha ya matamanio yake ya kuongeza mishahara lakini inamuwia vigumu kufanya hivyo kwa sasa.
"Ndugu zangu mimi ni mama na mama ni
mlezi ila kuna msemo usemao kuwa masikini huwa anapenda mwanae apendeze lakini
shida ni uwezo."
Rais Samia amesema ameshindwa kutimiza matamanio ya wafanyakazi
mwaka huu kwa kuwa kasi ya uchumi imeshuka na kwa Tanzania uchumi umeshuka
kutoka asilimia 6.9 mpaka asilimia 4.7 na hii inatokana na mlipuko wa janga la
corona.
Lakini amehaidi kupunguza kodi na tozo mbalimbali za serikali
kwa wafanyakazi. Aidha imemuwia vigumu kuongeza mshahara kwa kuwa ndio kwanza
anaanza kazi lakini mwakani ataweza kutimiza dai hilo ambalo ni mhimu kwa
wafanyakazi.
Kwa kutambua umuhimu
wa wafanyakazi amesema wanaenda kupandisha vyeo vya wafanyakazi 85,000 mpaka
91,000 ambao wataigharimu serikali milioni, wanakusudia kulipa malimbikizo ya
mishahara, kuboresha miundo ya kiutumishi na kuongeza ajira mpya takribani elfu
arobaini.
Vilevile wataongeza jitihada za kudhibiti mfumko wa bei za
bidhaa, hivyo anatumaini kwa jitihada hizo zitasaidia maisha ya watanzania.
Hata
hivyo wafanyakazi mkoani Rukwa wameungana na watu wengine dunia kote katika
kuadhimisha siku ya wafantakazi ambayo imefanyika kimkoa katika wilaya ya Kalambo.
Katika maadhimisho hayo shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania TUCTA kupitia risala limebainisha kuwa linaamini katika ushirikiano wa pamoja na mahusiano mema ndio ustawi wa taasisi zetu na nchi kwa ujumla na kwamba wote wanapaswa kuzingatia utawala wa sheria kwa kuzifuata ipasavyo ili itendeke kwa wanyakazi na vyama vingine.
Hali kadharika wafanyakazi mkoani humo walisistizwa kuwa msitari wa mbele katika kupinga na kukemea ajira za watoto majumbani .
Comments
Post a Comment