Na Baraka lusajo - Rukwa
Halmashauri ya Kalambo Mkoani Rukwa imeanza utekelezaji wa kuibua kaya masikini katika vijiji 45 ambavyo vilikuwa vimesalia katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango huo huku ikijidhatiti kuondoa wanufaika hewa kwa kuweka mfumo rafiki wa malipo ikiwa ni pamoja na kuangalia familia zenye watoto waliokosa misaada.
Katika
kipindi cha kwanza, vijiji na mitaa 9,960 sawa na 70% vilifikiwa , ambapo jumla
ya kaya milioni 1.36 zilitambuliwa na kati ya hizo kaya milioni 1.1 zenye jumla
ya watu milioni 5.4 ziliandikishwa kwenye masijala ya walengwa.
Hata hivyo katika kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF, kilizinduliwa rasmi, februali 17-2020 huku kipindi cha pili awamu ya tatu ya TASAF (PSSN 11) kilianza kutekelezwa mwaka 2020 hadi mwaka 2023 ambapo wilaya 184 za Tanzania bara na visiwani ikiwemo Unguja na Pemba ziliingizwa kwenye mfumo huo.
Hata
hivyo kwa wilaya ya Kalambo mpango huo umelenga kuvifikia vijiji 45 ambavyo
vilikuwa vimesalia katika awamu iliyopita, ambapo Halmashauri imeunda timu za wasimamizi
na wawezeshaji wa zoezi hilo katika vijiji hivyo.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Msongela Palela amebainisha
kuwa zoezi la utambuzi wa kaya utafanywa na wanajamii kupitia mikutano ya vijij/Mitaa
kwa usimamizi wa wawezeshaji kutoka kwenye mamlaka za maeneo husika.
Aidha Msongela alibainisha kuwa walengwa watakuwa ni kaya zinazoishi katika mazingira duni na hatarishi.
alisema licha ya hilo mpango utalenga kuwezesha kaya za walengwa kutumia furisa za kuongeza kipato ,huduma za jamii na kiuchumi na kuwekeza katika maendeleo ya watoto ambao ni rasilimali watu.
Alisema mpango huo utajikita zaidi kuwasaidia watoto wenye umri wa kwenda shule ambao wamekosa milo mitatu kwa siku na wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.
alisema licha ya hilo mpango huo utajikita zaidi katika kuwasaidia watoto ambao hawaendi kiliniki kupata huduma za afya .
“Vigezo
vya kaya za walengwa ni kaya ambazo zinakipato cha chini si cha uhakika
ukilinganisha na kaya zingine katika kijiji au mtaa, pia zitaangaliwa Zaidi kaya
ambazo hazimudu au hazina uhakika wa kupata milo mitatu kwa siku pamoja na
familia zenye makazi duni. Alisema Msongela’’
Kwa
upande wake kaimu mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa kunusuru Kaya masikini TASAF
nchini Beatrice Shemdoe,alisema kipindi cha pili awamu ya Tatu ya Mfuko wa
maendeleo ya jamii (TASAF II) kinatekelezwa katika Halmashauri 184 za Tanzania bara
na visiwani na kubainisha kuwa kipindi hiki kitafikia zaidi ya wananchi milioni
moja nchini kote.
“Mkazo
mkubwa katika kipindi chapili umewekwa katika kuziwezesha kaya masikini ili
kuziongezea kipato’’ alisema Shemdowe.
Alisema walengwa watakao tambuliwa na kuandikishwa katika kipindi cha pili ni kaya zinazoishi katika hali duni kwenye vijiji, mitaa na shehia na kwamba wanufaika ndani ya kaya watakuwa ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano wanao hudhuria kliniki.
Mkuu
wa wilaya hiyo Kalorius Misungwi aliwasisitiza watendaji kuwa waadilifu wakati
wa utekelezaji wa zoezi hilo na kuwasisitiza kufanya kazi kwa bidii kwa malengo
ya kupunguza umasikini na kuchochea ukuaji wa uchumi ukiwemo ule wa viwanda
ambayo ni ajenda muhimu ya serikali.
“Nitoe
ushauri kwa viongozi wenzangu, tunapofanya ziara zetu za kikazi katika maeneo yetu
tutenge muda wa kuongea na walengwa na kuwahamasisha kuanzisha miradi ya
ujasiriamali ili kukuza vipato vya kaya zao na kuwa na akiba ya kujikimu ili
hata pale ruzuku inapochelewa au kusitishwa wawe wamejiwekea misingi bora.
Alisema Misungwi.
Comments
Post a Comment