Halmashauari ya Kalambo mkoani Rukwa imefainikiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa katika shule ya Sekondari Mambwe iliyopo katika kata ya Ulumi na kuwawezesha wanafunzi 240 waliokuwa wamekosa nafasi kuendelea na masomo yao.
Shule ya sekondari Mambwe ilianzishwa rasmi
mwaka 1995 kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha nne, ambapo mpaka hivi ssa ina jumala ya wanafunzi
650 kwa kidato cha kwanza hadi cha
nne ikiwemo wavulana 372 na wasichana
278. Pia inawanafunzi 180 wa kidato cha tano na cha sita.
Afisa elimu Sekondari wilayani humo Jeshi Lupembe, alisema shule hiyo kabla
ya ujenzi wa madarasa matano shule ilikuwa na vyumba vya madarasa kumi na sita
kati mahitaji ya vyumba vya madarasa 20 na kufanya kuwa na upungufu wa vyumba
vya madarasa 4.
‘’Shule
hii inapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne kutoka kata mbili
ikiwemo kata ya Ulumi na Kata ya Mnamba ambayo haina shule ya sekondari ‘’Alisema
lupembe.
Kaimu afisa mipango wilayani humo Emily
Mwakalinga, alisema katika ujenzi huo, Halmashauri ili changia vifaa vya ujenzi
(saruji,mabao ,nondo,miusumari ,rangi,whiti
sement na bati) pamoja na kulipia gharama za ufundi na usafiri
na kughalimu fedha kiasi cha
shilingi 40,35,000.00.
Awali akikagua ukamilishwaji wa miradi
ya ujenzi wa shule hiyo katibu mkuu wa jumuiya ya serikali za mitaa (ALAT) Elirehema Kahoyo, aliwataka wananchi
kuendelea kujitolea nguvu zao na kuipongeza Hamashauri kwa kufanikiwa kutoa
miti 300 ya miti ya matunda na mbao kwa kila shule.
Comments
Post a Comment