Ijumaa Machi 26, 2021 wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watampumzisha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Dkt John Pombe Magufuli katika makazi ya milele huko Chato mkoani Geita wakiwa na huzuni na majonzi makubwa kumpoteza kiongozi wao aliyedumu madarakani kwa miaka mitano na siku 114.
Licha ya masikitiko yaliyowatawala, Rais Magufuli amewaachia zawadi na ndoto za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo itadumu kwa miaka mingi maishani mwao.
Kutamalaki kwa miradi iliyokamilika na inayoendelea kujengwa nchini humo na maelfu ya wananchi wakipanga barabarani, kujaa viwanjani huku vilio vikisikika sehemu mbalimbali kunaleta taswira pana juu ya uongozi wa Rais Magufuli jinsi ulivyowagusa baadhi ya wananchi hivyo vilio vyao ni kulilia tumaini lao.
Reli ya kisasa (SGR)
Tarehe 14 mwaka 2018
Rais John Magufuli aliasisi ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa kwa kuweka jiwe
la msingi la kipande cha pili cha mradi huo kilichoanzia mkoani Morogoro hadi
Makutupora mkoani Dodoma.
Kipande hicho chenye
urefu wa kilometa 422 kitagharimu kiasi cha shilingi trilioni4.3, ambapo ni
sehemu ya mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati wa kuanzia Dar es salaam hadi
Mwanza yenye urefu wa kilomita 1,219. Ujenzi wa kipande cha kutoka Dar es
salaam hadi Morogoro unaelezwa kuwa umekamilika kwa asilimia 80. Hii ni zawadi
aliyoacha Magufuli kwa Watanzania.
Mpango wa elimu bure
Serikali ya Magufuli
ilitekeleza mpango wa kutoa elimu bure kutoka shule za Msingi hadi sekondari na
kuwezesha maelfu ya wananchi kuwapeleka shule watoto wao. Elimu ni nyenzo ya
kuinua maisha ya wananchi na juhudi za serikali kuwaelimisha wananchi wake
zimeonekana ndani ya miaka mitano ya Magufuli. Wananchi wamepunguziwa mzigo
ambao uliwaelemea kwa miaka mingi kuanzia vijijini hadi mijini hivyo kuwa na
uhakika wa kupata elimu.
Vitambulisho vya Wamachinga
Julai 3, 2017 Rais
John Magufuli akiwa jijini Mwanza alisema hapendi kuwaona Wafanyabiashara
wadogo nchini Tanzania maarufu kama Wamachinga wakisumbuliwa na kushindwa
kufanya biashara zao. Ahadi yake ya kuhakikisha Wafanyabiashara hao wanafanya
kazi zao kwa uhuru ndizo kiini cha kupatikana kwa vitambulisho na huo ukawa
mwanzo wa uhuru wa Wamachinga na Wajasirimali wadogo kufanya biashara maenero
mbalimbali.
Aidha, uhuru waliopewa Wajasirimali wadogo umetokana na mpango
wa mpango wa MKURABITA, ambapo unainisha umuhimu wa kurasimisha biashara zisizo
rasmi mfano Mama Lishe, saluni, wamachinga na wafanyabiashara wengine wenye
mitaji ya chini ya shilingi milioni moja. Serikali ya Rais Magufuli ilitumia
mpango huo vizuri na kupata mafanikio kwa kusajili vijana wengi waliojihusisha
na biashara ya umachinga.
Umeme
bonde la Rufiji
TANESCO
Utekelezaji wa sera ya viwanda
Sera ya viwanda SIDP
(Sustainable Industrial Development Policy) ya mwaka 1996 inabainisha kuwa
Tanzania hadi mwaka 2015 ilitakiwa kuwa na viwanda vya kati. Sera hiyo
ilipitishwa na serikali ya awamu ya tatu ya serikali ya rais Benjamin Mkapa na
Waziri wa Viwanda na Biashara wa wakati huo alikuwa Dkt. Abdallah Kigoda. Hata
hivyo sera hiyo imepigiwa upatu na serikali ya Magufuli na kuwezesha ujenzi wa
viwanda mbalimbali vya uzalishaji, kutengeneza ajira, kukuza uchumi na pato la
taifa.
Ununuzi wa ndege
Kwa mujibu wa Ilani ya
CCM ya 2015-2020 imeelezea suala la matengenezo ya viwanja na kufufua Shirika
la Ndege (ATCL). Jumla ya ndege 11 zimenunuliwa na mamlaka za Tanzania.
Ndege ya shirika la ndege nchini Tanzania Air Tanzania
Matarajio ya ndege hizo ni kuongeza kiwango cha biashara ya
utalii nchini humo pamoja na shughuli zingine za kiuchumi.
Ang'arisha sekta ya afyA
Magufuli ameacha
zawadi ya zaidi ya vituo 400 vya afya ndani ya miaka mitano. Hospitali za
wilaya zaidi ya 70, Hospitali za rufaa za mikoa zaidi ya 10, Hospitali za rufaa
za Kanda ni tatu. Magufuli ameacha zawadi ya upandikizaji wa figo katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tangu mwaka 2017 huku zaidi ya wagonjwa 70
wamepatiwa huduma hiyo.
Hospitali ya Uhuru itakuwa kumbukumbu nyingine ya Magufuli kwa
wananchi wa Tanzania. Hospitali hiyo imeanza kutoa huduma kwa wakazi wa Dodoma
kwa baadhi ya magonjwa.
Baadhi ya viongozi wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Afya, Ummy
Mwalimu wamemwambia mwandishi wa makala haya kuwa mojawapo ya eneo ambalo
lilimkera Rais Magufuli ni kuona raia wake wakimiminika kwenda kutafuta matibabu
nje ya Tanzania hivyo alisisitiza lazima huduma za afya zipatikane kwa urahisi
nchini humo.
Rais Magufuli alipiga
vita rushwa na ubadhirifu tangu akiwa waziri hadi alipochukua mamlaka ya
kuongoza Tanzania mwaka 2015. Hatua madhubuti alizochukua ni pamoja na
kuanzisha mahakama maalumu ya kusikiliza kesi za ufisadi unaotendwa na watu
mbalimbali nchini mwake. Atakumbukwa kwa kupiga vita kivitendo.
Serikali ya Tanzania
ilidhibiti makinikia yaliyokuwa yanasafirishwa na kampuni ya madini ya Acacia
ambayo inamilikiwa na Barrick Gold. Makinikia ni mchanga uliokuwa unasafirishwa
kwenda kuchenjuliwa nje ya nchi jambo ambalo halikukubaliwa na uongozi wa
Magufuli.
RANDGOLD
Nguvu ya jiji la Dodoma
Wazo la aliyekuwa rais
wa kwanza wa Tanzania Julius Nyerere la kuhamisha makao makuu ya nchi kutoka
Dar es salaam kwenda Dodoma halikufanyika katika awamu tatu za marais wa nchi
hiyo hadi ujio wa Rais Magufuli aliyetangaza uamuzi wa kuhamisha makao hayo.
Halmashauri Kuu ya TANU (sasa CCM) ilipitisha mpango wa kuhamia
Dodoma chini ya Mwalimu Nyerere, lakini serikali hiyo haikuweza kutekeleza hadi
ilipoondoka madarakani mwaka 1984.
Tayari soko kubwa la kisasa limeshajengwa ambalo linaitwa Soko
la Job Ndugai ambalo linatarajiwa kuwavutia wengi na kuufanya Dodoma kuongeza
nguvu za kiuchumi.
Mradi wa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato-Dodoma ni zawadi
nyingine aliyoacha Magufuli na ambayo inaaminika Rais mpya Samia Suluhu Hassan
atakamilisha ndoto hiyo. Vilevile ndoto ya ujenzi wa mradi wa barabara ya njia
nne ya kilomita 112.3 ambayo inatarajiwa kupamba jiji la Dodoma.
Ujenzi wa uwanja wa michezo wa kisasa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 80,000 unatarajiwa kuwa kimbilio la watu wengi ndani na nje ya nchi. Upanuzi wa Ikulu ya Dodoma wenye eneo la mita za mraba 34,000 ni mradi mwingine ambao utakumbukwa kufanywa na Magufuli nchini mwake. Ingawa bado haujakamilika lakini ni miongoni mwa zawadi ambazo wameachiwa Watanzania.
Lugha ya Kiswahili
Uamuzi wa kutumia
lugha ya Kiswahili katika hotuba zake popote alipotembelea barani Afrika ni
zawadi nyingine. Katika moja ya ziara zake nchini Afrika kusini alipokwenda
kuhudhuria sherehe za kuapishwa rais Cyril Ramaphosa alishawishi nchi hiyo
kuchukua wataalamu wa kufundisha Kiswahili kutoka Tanzania. Katika ziara zote alikipigania
Kiswahili kuhakikisha kinatumika kama lugha rasmi na hivyo kuongeza idadi ya
wazungumzaji.
Hadi sasa Kiswahili ni lugha rasmi katika Jumuiya ya Afrika
mashariki,Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC).
Magufuli atakumbukwa kwa ushirikiano na nchi kama vile
Ethiopia,Afrika kusini na Morocco ambazo zilihitaji wataalamu wa lugha hiyo ili
kutoa elimu kwa wananchi wao. Alisaini makubaliano na Afrika kusini ya kutoa
wataalamu wa Kiswahili.
Mfupa
wa Mtwara Corridor
GETTY IMAGES
Aidha, ujenzi wa barabara ya Masasi-Songea-Mbinga. Awamu ya tatu
ya sasa ni kukamilika ujenzi wa kipande cha Mbinga hadi mji wa Mbamba Bay ambao
ni bandari inayounganisha nchi za Malawi na Msumbiji hivyo kusisimua uchumi wa
wananchi wa nchi hizo.
Kwenye ziara yake nchini Malawi Rais Magufuli aliwasilisha ombi kwa mwenyeji wake rais wa zamani Peter Mutharika na wananchi wa nchi hiyo kufanya biashara na ushirikiano mwema kwa sababu miundombinu ilikwishaboreshwa na kutumia vizuri bandari ya Mbamba Bay mkoani Ruvuma.
Miundo mbinu
Hadi mwaka 2017 pekee
serikali ya Magufuli ilifanikiwa kuunganisha mamlaka za Wilaya takribani 117,
vituo vya polisi 129 ,ufungaji wa taa za barabarani zinazotumia nguvu za
jua,kukarabati barabara zenye urefu wa kilomita 2,571 na ujenzi wa madaraja.
Magufuli alisimamia
ilani ya CCM (2015-2020) iliyosisitiza ukarabati na ujenzi wa viwanja vya ndege
katika mikoa mbalimbali. Wakati wa uongozi wake mradi wa Mabasi ya Mwendokasi
ulianza kutumika na kuwavutia maelfu pamoja na kutengeneza ajira kwa wananchi
wake. Utengenezaji wa vivuko vya maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, ujenzi wa vituo vipya vya mabasi vya kimkakati wa kupanua
miji vimejengwa katika mikoa mbalimbali. Vituo hivyo vinatajwa kuwa miongoni
mwa zawadi kubwa ambazo Magufuli amewaachia Watanzania kuanzia mikoa ya kusini
hadi kaskazini, kati hadi magharibi na pwani ambako imetengeneza fursa za ajira
na biashara.
Comments
Post a Comment