Philip Mpango aidhinishwa kuwa Makamu wa Rais Tanzania.

 

Bunge lamuidhinisha Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


 

Rais Samia Suluhu Hassan alimpendekeza Philip Mpango kuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Jina hilo liliwasilishwa bungeni asubuhi ya Jumanne na mpambe wa rais katika bahasha maalum.

 

Baada ya kupokea jina lake, Spika Job Ndugai alilitangazia bunge jina hilo lililopendekezwa na Rais Samia.

 

Spika Ndugai alilitangazia bunge hilo kuwa Dkt mpango amechaguliwa kwa kura 363 na baada ya kuchaguliwa kwa asilimia100%

Comments