Hayati Rais Magufuli Azikwa Nyumbani Kwake Chato

Hatimaye hayati John Pombe Magufuli Rais wa awamu ya tano wa Tanzania amezikwa katika makazi yake eneo la Mlimani Chato.Shughuli ya maziko iliyofanyika katika makaburi ya famila na kuhusiha watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, wastaafu na familia yake.Maelfu ya Watanzania wameshuhudia tukio hilo moja kwa moja kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya Tanzania.


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema, "Tunashukuru sana katika uongozi wake tumejifunza mengi, tumepikwa vizuri, tumeivaa haswa na tumeuiva sawa sawa. Tunapokwenda kumpumzisha tunaweza kusema bila kigugumizi, kuwa tuko tayari kuendeleza kazi yake nzuri kwa nguvu, kasi na ari ile ile."

Magufuli alifariki Machi 17 mwaka huu katika Hospitali ya Mzena mjini Dar es Salaam kwa matatizo ya moyo.

 



Comments