Hayati Rais magufuli awachia alama isio futika wakazi wa kalambo.



Siku moja kabla ya mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli kupumzishwa katika nyumba yake ya milele huko kijijini kwao Chato. Shughuli zilianzia Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mwanza na hatimaye zinamalizikia Chato Kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Maombolezo yanaendelea na shughuli za nchi zimesimama. Bado kuna vilio na huzuni. Salamu za rambirambi zinamiminika kutoka ndani na nje ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Watanzania wamepewa fursa ya kumuaga.

 

Mtawala anapofariki, kinachosalia ni kumbukumbu. Watanzania wanayo mengi ya kumkumbuka Magufuli kwa utawala wake wa miaka mitano na miezi kadhaa.

"Mwanamapinduzi," "mtoto wa bara la Afrika," Mwafrika wa kweli," shujaa dhidi ya ufisadi." Ni kauli kutoka marais wa Afrika waliohudhuria shughuli ya kumuaga katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Wengi wanamkumbuka kama mtetezi wa Tanzania. Kiongozi aliyepigania maendeleo ya watu wake na kupambana na rushwa na ufisadi. Hakuvumilia wateule wake waliofanya uzembe na kutowajibika.

 

Yamkini ndani ya Afrika Magufuli alivutia wengi kwa uongozi wake uliojikita kuwatumikia Watanzania masikini. Akipambana na mianya ya matumizi mabaya ya pesa za umma, ubadhirifu na ufujaji.

Kiongozi aliyeipenda nchi yake kiasi cha kutofanya safari yoyote nje ya bara hilo. Daima aliwakilishwa na mabalozi, mawaziri au Makamu wake. Alibaki ndani ya Tanzania akihudumia raia wake. Licha ya hilo wananchi katika mikoa mbalimbali wameendelea kufanya maombi dhidi ya kiongozi huyo huku wengi wao wakielezea kumkumbuka daima kutokana na alama kubwa alioiacha ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara na ujenzi wa vituo vya afya.


Hata hivyo katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wakaziwa wilaya hiyo Machi 24/2021 walifanya maombi ya kumuombea kwa mungu hayati Rais magufuli na kuelezea kumkumbuka daima kutokana na kupigania ujenzi wa vituo vitatu vya afya, Hosptari ya wilaya pamoja na ukamilishwaji wa barabara ya lami kutoka Sumbawanga hadi Kasanga


Licha ya hilo wakazi wa wilaya hiyo wameelezea kumkumbuka Rais magufuli kwa kuanzisha ujenzi wa bandari ya Kasanga pamoja na kuimalisha miundombinu ya barabara katika mji wa Matai.


Maoambi hayo yaliofanyika wilayani humo katika soko kuu la mazao (matai) yalishirikishwa na viongozi wa dini, viongozi wa kimira ,wakuu wa idara ,kamati ya ulinzi na usama pamoja na viongozi wa kisiasa.


Comments