Rais wa Tanzania John
Pombe Magufuli amewataka watanzania kutumia dawa za asili katika mapambano
dhidi ya Covid-19
Akizungumza Jijini Dodoma
hii leo, amesisita juu ya matumizi ya miti shamba pia kujifukiza katika
mapambano dhidi ya Covid-19.
Aidha amesema kuwa si
kila dawa zinazotoka nje ya nchi ni nzuri kwa watanzania.
''Kuna dawa inaitwa
Covidol, Bugiji zinafanya kazi kwasababu zimekua proved na mkemia mkuu, kamwe
msifikirie kila dawa inayotoka nje ni kwa ajili yenu, ingekua hivyo Malaria
ingeisha. Tujitambue tusitumike. Madawa haya yalipigwa vita na wakoloni
kwasababu ya uchumi, ukiwa na mti wako hata kama unaponesha malaria utaambiwa
ni wa kishamba''. Alisema Magufuli
Ameitaka pia Wizara ya
Afya kutoa ushirikiano kwa wagunduzi wa dawa za asili.
''Mungu ametupatia hii
mimea na ikabarikiwa, tuitumie, lakini tuitumie kwa kufuata masharti na
utaalamu mzuri, kwa hiyo Taasisi yetu ya Wizara ya Afya inayosimamia dawa za
asili, huu ni wakati wa kuyatumia kikamilifu. Na Wizara ya Afya isiwakatishe
tamaa watu hawa, na madaktari wanatumia hizo hizo dawa, wao wanaenda
wanakunywa, wanajifukiza wakija huku wanawatwanga masindano'' Alisema.
Ameongeza pia kuwa
Watanzania kwa wakati wote wamemtanguliza Mungu na kuendelea kujilinda hivyo
wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari.
Viongozi wa ngazi
mbalimbali pia wameendelea kuhamasisha matumizi ya dawa asili katika mapambano
ya Covid-19.
Comments
Post a Comment