Kalambo Kutunga Sheria Ndogo Kudhibiti Utoro Wa Wanafunzi Mashuleni.

Na Baraka Lusajo- Kalambo 

Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa imeanza kuchukua hatua za kukomesha vitendo vya utoro mashuleni kwa kutunga sheria ndogo zitakazo saidia kuwachukulia hatua wazazi na walezi wanaoshindwa kuchangia vyakula kutokana na shule 14 kati ya 15 za sekondari kutoa chakula kwa asilmia 60 huku shule 98 za msingi zikishindwa kutekeleza zoezi hilo na kusababisha kujitokeza mdondoko mkubwa na utoro kwa wanafunzi wilayani humo.

 Hayo Yanajiri Kupitia Kikao Cha Ushauri Cha Wilaya (DCC) Ambapo Wazazi Na Walezi Wilayani Humo Wametajwa Kuwa Chanzo Cha Watoto Kuto Pata Chakula Kwa Asimia 100 Shuleni kutokana na mwamko mdogo wa elimu.


Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya hiyo Msongela palela, alisema hali ya utoaji chakula mashuleni imekuwa siyo ya kuridhisha kwani ni asilimia 60 pekee ya wanafunzi wanaopata chakula katika shule 14 kati ya 15 za sekondari hali ambayo imekuwa ikipelekea ujifunzaji na ufundishaji kuathirika na kusababisha mdondoko wa wanafunzi kuwa mkubwa.


Alisema Halmashauri imeanza kutunga sheria ndogo na kusimamia sheria zitakazo mtaka mzazi kuwajibika kwa mtoto wake ikiwa ni pamoja na kuchangia chakula shuleni na kusimamia mahudhurio yake pindi awapo shuleni.

‘’Kupitia kikao hiki wadau wote wa elimu tuungane kutoa hamasa kwa jamii kuona umuhimu wa kuchangia chakula na kusimamia mahudhurio ya watoto wetu wawapo shuleni ‘’alisema Msongela.


Mkuu wa wilaya hiyo Kalorius Misungwi aliwahimiza watendaji pamoja na maafisa elimu kuhakikisha kamati za shule zinaanza kufanya kazi kwa mujibu wa sheria  na kusisitiza kuhakikisha wanachagua viongozi wa kamati ambao wanauelewa  dhidi ya masuala ya elimu.

Halmashauri ya kalambo inajumla ya shule za sekondari 19 zenye jumla ya wanafunzi 8,117. Shule 15 za serikali na zisizo za serikali huku shule za msingi zikiwa ni 98.

 

Comments