Wahitimu Wa Mafunzo Ya Kijeshi Waonywa Kutojihusisha Na Vitendo Viovu


Wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kupitia jeshi la akiba wilayani kalambo mkoani  Rukwa wameonywa kutojihusisha na vitendo viovu pindi watakapo rudi uraiani na kusisitizwa kujikita zaidi katika shughuli za uzalishaji mali na kulinda raia na mali zao.

Mafunzo hayo ya mehusisha wahitimu wapatao 134 kati yao wanaume 99 na wanawake 35 huku wakitakiwa kuwa raia wema na kichocheo cha amani na utulivu wilayani kalambo na taifa kwa ujumla.



Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu hao Jen Ngonyani, amesema kupitia mafunzo hayo wamejifunza mbinu mbalimbali za kivita kwa nadhraia na vitendo vikiwemo usomani ramani, utimamu wa mwili, nidhamu na uzalendo huku wakiiomba serikali kuweka utaratibu maalumu utakao wawezesha kupata ajira za kudumu na za muda ili kunufaika kiuchumi.


licha ya hilo, wameiomba serikali kuongeza muda wa mafunzo kwani muda  uliowekwa ni mdogo na  hivyo kushindwa  kujifunza baadhi  ya masomo mengi yakiwemo matumizi ya aina nyingi za siraha.

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo wakati wa kufunga mafunzo, katibu tawala wa wilaya Frank Sichalwe akawataka wahitimu hao kuyatumia mafunzo hayo  kuwakamata wahalifu wote.


Aidha amewaagiza watendaji wa  vijiji na kata  kuhakikisha wanashirikiana na askari  hao katika kuwabaini  waharifu  wakiwemo watu  wanaolewa wakati wa saa za kazi.

Kwa upande wake mshari wa mgambo wilayani humo  meja  Gwamaka Mwailunga, amesema mafunzo hayo yalianza julai 13 ,2020 na kuhitimishwa leo julai 17, 2020, mafunzo yaliyodumu kwa muda wa  miezi mitano tangu kuanza kwake.


Amesema mafunzo  hayo yatakuwa mwarobaini wa kukomesha matukio ya wizi  kwa baadhi ya maeneo ambayo asikari hawafiki kwa  urahisi na  kuwataka  wahitimu hao  kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa  kujikita  katika  shughuli za uzalishaji  mali zikiwemo za kilimo.

Comments