Rais Magufuli Afungua Rasmi Bunge La 12 Tanzania



Rais wa Tanzania, John Magufuli amefungua Bunge la 12 mjini Dodoma na kulihutubia Bunge hii leo.

Akiwahutubia wabunge hii leo, Magufuli ametoa dira ya serikali yake baada ya kumaliza awamu ya kwanza.

Rais Magufuli amesema mambo muhimu anayoyapa kipaumbele katika miaka mitano ijayo ni;

Kuendelea kulinda na kudumisha tunu za taifa, yaani amani, umoja na mshikamano , uhuru wa nchi, Muungano na mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

'' Katika hilo ninaahidi kushirikiana kwa ukaribu sana na Rais mpya wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi. Kamwe hatutakuwa na mzaha na yeyote mwenye kutaka kuhatarisha amani ya nchi yetu. Mwenye nia ya kuvuruga umoja na mshikamano wetu, pia mwenye kutaka kutishia uhuru wetu, Muungano pamoja na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar." alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemuahidi Dkt Hussein Mwinyi kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itafanya kazi kwa karibu sana na Serikali ya Zanzibar ili kuleta maendeleo kwa pande zote mbili za Muungano.

 

Comments